Taarifa ya Jeshi la Israeli iliyochapishwa saa kadhaa baada ya ving’ora kusikika katika jamii za Israeli zinazopakana na Lebanon, ilisema zaidi ya makombora 40 yalionekana yakivuka mpaka kutoka Lebanon, baadhi yake yalitunguliwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya jeshi la Israeli na hakuna yaliyosababisha majeruhi.
Siku ya Jumatano (Mei 15), Hezbollah ilisema imefanya shambulizi la droni katika kituo cha kijeshi magharibi mwa Israel huko Tiberias ikiwa ni shambulizi la ndani zaidi katika eneo la Israeli tangu kikundi chenye silaha cha Lebanon kilipopambana na Israel sambamba na vita vya Gaza
Mashambulizi hayo yalijeruhi wanajeshi watatu, moja wao akiwa katika hali mbaya, kulingana na jeshi la Israeli.
Mara nyingi Hezbollah imekuwa ikishambulia upande wa pili wa mpakani na Israel kwa zaidi ya miezi saba iliyopita, lakini shambulizi la Alhamisi lilionekana kuwa ni la kwanza la kombora lililokuwa na mafanikio iliyofanya katika anga ya Israeli.
Kundi hilo limeongeza mashambulizi dhidi ya Israel katika wiki za hivi karibuni, hususan tangu Israeli ilipovamia mji wa Rafah uliopo upande wa kusini wa Ukanda wa Gaza. Imefanya shambulizi la ndani zaidi nchini Israel na kuanza kutumia silaha mpya na za kisasa zaidi.
“Hii ni njia ya kufikisha ujumbe kwa adui Israel katika uwanja wa vita, ikimaanisha kuwa hiki ndicho tuliokuwa nacho, na ikihitajika tunaweza kushambulia zaidi,” alisema mchambuzi wa kisiasa wa Lebanon Faisal Abdul-Sater ambaye anaifuatilia Hezbollah kwa karibu.