Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 02:32

Katibu Mkuu wa UN anasikitishwa na harakati za kijeshi zinazoendelea Rafah


Antonio Gutteres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Antonio Gutteres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Wapalestina 450,000 wamelazimika kuyahama makazi yao katika eneo la Rafah katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema Jumanne amesikitishwa na kuongezeka kwa harakati za kijeshi, ndani na kuzunguka mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah, zinazofanywa na vikosi vya ulinzi vya Israel, wakati Wapalestina 450,000 wamelazimika kuyahama makazi yao katika eneo hilo katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

“Maendeleo haya yanazuia zaidi upatikanaji wa misaada ya kibinadamu na kuifanya hali kuwa mbaya zaini”, naibu msemaji wake Farhan Haq aliwaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa. “Wakati huo huo, Hamas inaendelea kurusha roketi kiholela. Raia lazima waheshimiwe na kulindwa wakati wote, katika Rafah na kwingineko huko Gaza”.

Kwa wiki moja iliyopita, jeshi la Israel limezidisha mashambulizi ya mabomu na operesheni nyingine katika mji wa Rafah huku likiamuru watu kuondoka katika sehemu za mji huo. Israel inasema inafanya operesheni ndogo ya kuharibu miundombinu ya wanamgambo katika mpaka wa Gaza na Misri.

Forum

XS
SM
MD
LG