Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Russia Vladimir Putin walikuwa wa mwisho kuwasili katika sherehe hizo zilizofanyika Paris, Ufaransa. Wawili hao walipeana mikono na Putin alinyanyua dole gumba juu kuitikia salamu ya Trump “Vipi hali yako?”
Katika hotuba yake Macron ameeleza kujitoa muhanga watu hawa waliouwawa katika vita miaka mia moja iliopita katika kipindi cha miaka minne ya mauaji ya kinyama huko Ulaya.
“Uaminifu ni msimamo ambao ni kinyume cha ubaguzi,” amesema Macron. “Ubaguzi ni usaliti dhidi ya uzalendo.”
Mapepo ya zamani yanaamka, yakiwa tayari kupandikiza mbegu za chuki na mauaji,” ameonya Rais Macron.
“Historia wakati mwengine inatishia kurejea kwa maafa mbalimbali na kukandamizi urithi wa amani ambao tulikuwa tunafikiria tumekwisha kamilisha kwa damu iliyokuwa imemwagika kwa kujitolea muhanga wahenga wetu.”