Gallup : Shambulio la Septemba 11 bado linawaathiri Wamarekani

Kituo cha Kimataifa cha Biashara, Marekani kufuatia shambuizi la kigaidi lililofanywa na ndege iliyokuwa imetekwa huko New York City, Septemba 11, 2001.REUTERS/Sean Adair SV

Wakati Marekani  ikikaribia kumbukumbu ya miaka 20 ya shambulio la kigaidi la September 11 lililoua takriban watu 3,000, Wamarekani wengi wanasema tukio hilo bado linaathiri maisha yao, utafiti wa Gallup unaonyesha.

Utafiti huo uligundua leo kuwa asilimia 26 ya Wamarekani wanaonyesha kusita kuruka kwenye ndege , asilimia 27 wanahisi vivyo hivyo juu ya kuingia kwenye majengo marefu sana, na asilimia 36 wanahisi hivyo hivyo juu ya kusafiri nje ya nchi. Asilimia 37 walikuwa na wasiwasi juu ya kuhudhuria hafla zinazojumuisha umati mkubwa.

Mara tu baada ya mashambulio hayo, nambari hizo zilikuwa asilimia 43, 35, 48 na mtawalia.

Wamarekani wenye kipato cha chini wenye umri zaidi ya miaka 50 na bila shahada ya chuo kikuu walikuwa na uwezekano mkubwa wa kuhisi kusita juu ya kushiriki katika hafla hizo.

Na utafiti uliofanywa kabla ya mashambulizi mabaya katika uwanja wa ndege wa Kabul mnamo Agosti 26, pia uligundua Wamarekani walikuwa na uwezekano mdogo wa kusema Amerika inashinda vita dhidi ya ugaidi.