Ni wadhifa ambao hauna madaraka ya kiutendaji nchini Ethiopia. Hata hivyo, msemaji wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed ameeleza hatua hiyo ni ya “kihistoria”na amesema inaonyesha kuwa wanawake watakuwa na mchango muhimu katika siasa za Ethiopia. Hili limejiri baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Mulatu Teshome, kujiuzulu ghafla.
Kuteuliwa kwa Sahle katika nafasi hiyo Alhamisi inafuatia mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliofanywa na Waziri Mkuu Abiy Ahmed na kufanya wanawake kufikia idadi ya asilimia 50 katika nafasi za juu za uwaziri.
Hivi sasa wanawake wanashikilia asilimia 37 za viti vya bunge la Ethiopia, na ni mara dufu ya idadi ya wanawake walioko katika Bunge la Marekani.
Haijawahi kutokea huko nyuma wanawake wa Ethiopia kushikilia nafasi za juu serikalini.
Lakini kukosekana usawa wa jinsia ni jambo lililo wazi na linaendelea kuwepo nchini, na haijulikani vipi maboresho katika uwakilishi wa wanawake katika serikali kuu yatakuwa na athari kwa nafasi ya zaidi ya wanawake na wasichana milioni 50 nchini Ethiopia.
Baada ya kuapishwa kushikilia nafasi hiyo Alhamisi, Sahle-Work amesema anaona nafasi yake ni muhimu kwa wanawake katika kutatua changamoto kubwa zilizoko katika jamii, ndani ya Ethiopia na sehemu nyingine.
“Iwapo mageuzi tulio yaanzisha yataweza kuwashirikisha wanawake na wanaume ili kuleta usawa, nchi muda simrefu itasahau hali ya umaskini na kutokuwepo maendeleo na kuelekea kwenye mafanikio,” amesema.
Sahle-Work ni mwanadiplomasia mwenye uzoefu ambaye sasa amekuwa kiongozi wa kipekee mkuu mwanamke barani Afrika.
Katika hotuba yake ya kukubali wadhifa huo, Rais Sahle-Work, amezungumza kuhusu umuhimu wa kudumisha amani.
Rais Sahle-Work amewahi kuwa Balozi wa Ethiopia nchini Senegal na Djibouti na amewahi kushika nyadhifa kadhaa katika Umoja wa Mataifa ikiwamo Mkuu wa Kujenga Amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.