Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 18:55

Milipuko miwili yalenga viongozi wa Ethiopia, Zimbabwe


Watu waliojeruhiwa baada ya mlipuko uliotokea mjini Bulawayo, Zimbabwe, 23 Juni, 2018.
Watu waliojeruhiwa baada ya mlipuko uliotokea mjini Bulawayo, Zimbabwe, 23 Juni, 2018.

Milipuko miwili tofauti iliwayolenga viongozi wa Ethiopia na Zimabwe ilitokea katika mazingira yaliyowiana lakini kwenye miji miwili tofauti.

Milipuko hiyo ilitokea Jumamosi muda mfupi baada ya Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, na rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, kuhutubia mikutano ya kisiasa mijini Addis Ababa na Bulawayo mtawalia.

Hata hivyo, hakukuwa ishara yoyote mashambulizi hayo yalikuwa na uhusiano wa moja kwa moja.

Huko Zimbabwe, mlipuko mkubwa ulitokea kwenye uwanja wa michezo mjini Bulawayo, muda mfupi baada ya rais wa nchi hiyo, Emerson Mnangagwa kuhutubia mkutano wa kisiasa.

Msemaji wa Mnangagwa alinukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema kuwa rais huyo hakujeruhiwa licha ya kwamba mlipuko huo ulitokea karibu na mahali alipokuwa akiwapungia mkono wafuasi wake.

Video ya kituo cha televisheni cha taifa ilionyesha mlipuko huo ukitokea karibu na Mnangagwa ambaye alikuwa anatembea kutoka kwa jukwa akirejea kwenye hema walipoketi wageni mashuhuri huku akiwapungia mkono waliohudhuria mkutano huo.

Zimbabwe inatarajiwa kufanya uchaguzi wa urais tarehe 30 mwezi ujao. Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 75 anawania kiti hicho chini ya chama kinachotawala cha Zanu PF, dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Nelson Chamisa, mwenye umri wa miaka 40, anayewania chini ya chama cha upinzani cah Movement for Democratic Change (MDC).

Mlipuko iliotokea nchini Zimbabwe Jumamosi tarehe 23 Juni, 2018.
Mlipuko iliotokea nchini Zimbabwe Jumamosi tarehe 23 Juni, 2018.

Mapema Jumamosi nchini Ethiopia, mtu mmoja aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati wa mkutano wa kisiasa uliohuhuriwa na halaiki na kuhutubiwa na waziri mkuu wa nchi hiyo, Abiy Ahmed, katika mji mkuu, Addis Ababa.

Kiongozi huyo ambaye ameleta mabadiliko makubwa ya kiutawala, alikuwa tu amemaliza kutoa hotuba yake wakati nguruneti hiyo ilipolipuka.

Abiy baadaye alidai kuwa shambulizi hilo lilikuwa limepangwa na kwamba polisi walikuwa wameanza kuchunguza ni nani waliohusika.

Katika mahojiano ya televisheni siku ya Jumamosi, waziri mkuu Abiy alisema upendo utashinda,

"Kujaribu kuwaua watu ni kuonyesha ni ishara ya udhaifu. Wale waliojaribu kuwagawanya Waethiopia hawakufaulu," aliongeza.

Abiy alichukua usukani mwezi Aprili na kulingana na Reuters, amefanya mabadiliko mengi, ikiwa ni pamoja na kuwaachilia wafungwa wa kisiasa na waandishi wa habari.

Aidha, ameanza mikakati ya uimarishaji wa uchumi huru na kuahidi kutafuta mwafaka wa amani kati ya Ethiopia na hasimu wake, Eritrea.

XS
SM
MD
LG