EAC: Somalia yawasilisha ombi la kuimarisha mifumo ya kimahakama

Jaji mkuu wa Somalia Yusuph Bashe Mohamed amewasilisha ombi maalum Kwa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuisaidia Somalia

Jaji mkuu wa Somalia Yusuph Bashe Mohamed amewasilisha ombi maalum Kwa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuisaidia Somalia kuimarisha mifumo ya kimahakama ambayo imeathiriwa na vita hatua itakayoharakisha mchakato unaoendelea wa nchi hiyo wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Jaji mkuu wa Somalia Yusuph Bashe Mohamed amewasilisha ombi maalum Kwa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuisaidia Somalia kuimarisha mifumo ya kimahakama ambayo imeathiriwa na vita hatua itakayoharakisha mchakato unaoendelea wa nchi hiyo wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Jaji Mkuu aliwasilisha ombi hilo katika Mkutano wa pili wa Majaji wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unaoendelea katika jiji la Kampala nchini Uganda ukishirikisha pia majaji wa mahakama za ndani na nje ya nchi za Jumuiya hiyo.

Mkutano wa pili wa Majaji wa Mahakama, Jumuiya ya Afrika Mashariki,unaoendelea katika jiji la Kampala nchini Uganda. Picha na Asraji Mvungi

Amesema mifumo ya mahakama ikiimarika itaongeza upatikanaji wa haki suala ambalo litawawezesha wananchi kuongeza imani kwa serikali na kwamba wana imani ya kupata msaada kutoka katika jumuiya hiyo .

Suala hilo limezungumziwa na baadhi ya majaji akiwemo Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki Nestor Kayobera ambaye amesema licha ya kuwa ni jambo jema linahitaji kupitia kwa ngazi zinazohusika

Aidha Jaji Kayobera ametoa mfano wa kufuata taratibu kama zinazoendelea katika nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambayo licha ya sasa kuwa ni mwanachama bado taratibu zinaendelea

Kayobera: “…Mfano utaratibu unaendelea nchini DRC ambayo licha ya kuwa ni mwanachama lakini bado kuna mambo yanaendelea kufanyika kukamilisha taratibu”

Kwa upande wake Waziri amesema kwa sasa mchakato wa ombi la Somalia kujiunga na jumuiya hiyo unaendelea katika ngazi mbalimbali.

Kadaga ameeleza kuwa: “.Ombi la somalia kujiunga linaendelea kupitiwa na ngazi zinazohusika.

Baada ya DRC kujiunga na jumuiya hiyo, Somalia pia imeshatuma maombi ya kutaka kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki maombi ambayo hivi karibuni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki alikaririwa akisema kwamba yanaendelea kufanyiwa kazi.

Kama Somalia ikifanikiwa kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Masharik, jumuiya hiyo ya kikanda itakuwa na jumla ya nchi nane wanachama hatua ambayo wadau wa maendeleo wanasema inatarajiwa kuongeza ustawi na usalama wa nchi za ukanda huo .

Imetayarishwa na mwandishi wetu Asraji Mvungi, Kampala, Uganda