Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:02

Nchi washiriki zavutana nani awe mwenyeji wa benki kuu ya Afrika Mashariki


Marais Uhuru Kenyatta na mwenzake Yoweri Kaguta Museveni
Marais Uhuru Kenyatta na mwenzake Yoweri Kaguta Museveni

Gazeti la East African limepata taarifa kuwa Kenya na Uganda walikataa uamuzi wa zoezi la uhakiki lililotakiwa kufanyika ili kutafuta nchi iliyo bora kuwa mwenyeji wa taasisi hiyo, ambayo iliichagua Tanzania.

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliwasilisha maombi yao ya kuwa mwenyeji wa taasisi hiyo ambayo baadae itapelekea kuwepo Benki Kuu ya kanda.

Lakini EAMI imekuwa ni kitu chenye mvutano, ambapo nchi wanachama wanashindana kila mmoja kuwa mwenyeji wake, wakijiweka vizuri kupata kivutio cha uwekezaji mkubwa wa mtaji wa kigeni na kufikia kuwa kituo cha fedha cha kieneo.

Gazeti la East African limepata taarifa kuwa Kenya na Uganda walikataa uamuzi wa zoezi la uhakiki lililotakiwa kufanyika ili kutafuta nchi iliyo bora kuwa mwenyeji wa taasisi hiyo, ambayo iliichagua Tanzania.

Washirika hao wawili walihoji lengo la zoezi hilo. Wakati wa mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri uliofanyika Arusha, Tanzania wiki mbili zilizopita, kutokukubaliana kulipelekea kusitishwa kwa majadiliano juu ya kuchagua nchi itakayokuwa mwenyeji wa EAMI.

Uhakiki ulifanyika mwezi Machi mwaka 2022 uliiweka Tanzania katika nafasi nzuri zaidi kuwa mwenyeji wa taasisi hiyo ikipewa asilimia 86.3, ikifuatiwa na Uganda (asilimia 82.42) na Burundi (asilimia 78.1). Kenya ilipata asilimia ya chini zaidi ya 77.35. Wanachama wengine hawakuonyesha utashi wa kuwa wenyeji.

Ripoti ya Baraza la EAC ambayo gazeti la The East African iliiona inaonyesha kuwa Uganda haijaridhishwa na ripoti hiyo ya kamati ya uhakiki “ na wanapendelea suala hilo lipelekwe ngazi ya juu zaidi.”

Chanzo cha habari hii ni gazeti la “The East African”

XS
SM
MD
LG