Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 01:23

EAC yarasimu muongozo wa kuhamisha pensheni kati ya nchi wanachama


Rais William Ruto
Rais William Ruto

Umuhimu wa mageuzi hayo uligusiwa na Rais wa Kenya William Ruto, aliyewasilisha mapendekezo kwa kuufanyia mageuzi Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Kenya (NSSF).

Wafanyakazi katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki huenda siku za karibuni wataweza kuhamisha mafao ya pensheni walizonazo kutoka nchi moja kwenda nyingine, wakihakikishiwa kutopoteza chochote hata kama mtu ataamua kubadilisha kazi.

Hii ni sehemu ya mapendekezo kwa jumuiya hiyo kuungana na kuufanya mfuko wa mafao ya pensheni kuwavutia wafanyakazi ambao hadi sasa wamekuwa wakidunduliza akiba zao katika mfuko wa hifadhi ya taifa au binafsi katika nchi wanakofanya kazi.

Umuhimu wa mageuzi hayo uligusiwa na Rais wa Kenya William Ruto, aliyewasilisha mapendekezo kwa kuufanyia mageuzi Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Kenya (NSSF).

Pendekezo moja ni kufanya iwe ni wajibu kwa yeyote mwenye kipato cha kila siku kuchangia katika mfuko huo kwa ajili ya mafao yao bila ya kujali makubaliano ya mkataba wao, na pia kufanya ni wajibu wa waajiri kuchangia kiwango sawa na kile kilichochangiwa na wafanyakazi.

“Tunakusudia kubadilisha miundo mbinu ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii ili uweze kumshirikisha kila mtu. Kuwapa moyo wale waliokuwa hawakushirikishwa kuweka akiba, Nitapendekeza ushawishi wa uwekaji akiba kitaifa kuwahamasisha wale walioko katika sekta isiyokuwa rasmi wajiwekee mpango wa kuweka akiba wa mafao ya kustaafu,” alisema Rais Ruto katika hotuba yake ya mabunge mawili wiki mbili zilizopita.

XS
SM
MD
LG