Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:55

Mkakati mpya kutumika katika kupeleka jeshi la kikanda la Afrika Mashariki DRC


Kituo cha jeshi la kulinda amani la MONUSCO Goma kikiwaka moto baada ya kuchomwa na waandamanaji, mwezi wa Julai 2022.
Kituo cha jeshi la kulinda amani la MONUSCO Goma kikiwaka moto baada ya kuchomwa na waandamanaji, mwezi wa Julai 2022.

Kupelekwa karibuni kwa jeshi la kikanda la Afrika Mashariki katika sehemu za mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutafanyika baada ya kampeni ya kuwafahamisha wananchi wote kuwepo wa jeshi hilo.

Maafisa wanasema kwanza wanataka kusahihisha makosa ya siku za nyuma yaliyofanywa na vikosi vya ulinzi vya kimataifa vingine, kwa kuwaelimisha raia kuhusu jukumu la majeshi hayo, ikiwemo kushauriana na wenyeji juu ya kuachana na vita.

Hii ni mbinu mpya iliyopitishwa wiki iliyopita Kinshasa kusaidia kujenga programu ya amani katika hali iliyokuwa haina utata.

Christophe Lutundula, Makamu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC wiki iliyopita alisaini mikataba kadhaa juu ya majukumu ya jeshi la kikanda na Peter Mathuki, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, inayoruhusu nchi wanachama kupeleka majeshi yake mara moja.

Lakini wakati ni suala la muda tu kwa majeshi kuwasili nchini humo, wakuu wa majeshi kutoka nchi wanachama walikubaliana kwamba malengo makuu ya peresheni zao ni kutoa nafasi zaidi ya kuhusishwa kwa raia katika operesheni hizi.

Walikubaliana kuwa kuwepo kwa majeshi yaliyopelekwa na UN na Jumuiya ya SADC yalikabiliwa siku zote na kutiliwa mashaka na umma.

Na kwa Umoja wa Mataifa, majeshi siku za nyuma yametuhumiwa kuhusika na mauaji ikiwemo ubakaji.

Tangu mwezi Julai, waandamanaji wamekuwa wakilenga kambi za walinda amani wa UN huko mashariki mwa DRC, wakiwatuhumu kushindwa kwao kuwadhibiti waasi.

Kikosi hicho cha dharura cha EAC kitakuwa awali na muda maalum wa miezi sita, utakaoongezwa, na mbali na kupambana, kitafanya kazi kuunda programu za kiraia kama vile kuweka vituo vya kijamii na kufanya mikutano ya amani na wanavijiji katika mkakati mpya unaokusudia kuwaweka wananchi karibu na maafisa wao.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African" linalochapishwa Kenya

XS
SM
MD
LG