Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:35

DRC: Watu kadhaa wafariki katika mlipuko wa lori la mafuta


Ramani ya DRC
Ramani ya DRC

Watu kadhaa wamefariki na wengine wameungua vibaya wakati lori la mafuta lilipolipuka katika kijiji kimoja magharibi mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mkuu wa jimbo amesema Alhamisi.

Mlipuko huo ulitokea usiku wa kuamikia leo Alhamisi katika kijiji cha Mbuba, umbali wa kilomita 120 magharibi mwa mji mkuu Kinshasa, gavana wa jimbo la Congo ya kati Guy Bandu ameandika kwenye twitter.

Zaidi ya watu 50 walifariki katika mlipuko wa lori la mafuta katika kijiji hicho hicho mwezi Oktoba mwaka wa 2018.

Kijiji cha Mbuba kinapatikana kwenye barabara kuu RN1 yenye shughuli nyingi inayounganisha Kinshasa na bandari za Matadi na Boma.

“Ni wakati muafaka wa kuchukua hatua kali na za kijasiri ili kuimarisha kanuni za usafiri, hasa kwa bidhaa zinazoweza kuwaka ili kukomesha ajali hizi za mara kwa mara,” Bandu amesema.

Ameongeza kuwa barabara hiyo kuu haipaswi kuwa kaburi.

XS
SM
MD
LG