Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:52

Kundi la ADF lafanya mauaji ya raia 5 wa DRC


Jeshi la DRC likiwa katika moja ya oparesheni zake kukabiliana na kundi la ADF mashariki mwa DRC.
Jeshi la DRC likiwa katika moja ya oparesheni zake kukabiliana na kundi la ADF mashariki mwa DRC.

Kundi la wanamgambo la ADF limeua raia watano mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, jeshi na maafisa wa nchini humo wamesema Alhamisi katika ghasia za karibuni kabisa katika eneo hilo.

Shambulizi limetokea Jumatano usiku katika eneo la Bulungo la Kivu Kaskazini, amesema msemaji wa jeshi la DRC Kapteni Antony Mualushayi.

Baada ya mapambano na jeshi wanamgambo hao wenye msimamo mkali walikimbia lakini baada ya kuwachinja raia watano waliokuwa wanawashikilia mateka amesema.

Kundi la ADF ambalo kundi la kigaidi la Islamic State imelitangaza kama mwakilishi wake wa Afrika ya Kati, ni miongoni mwa makundi mabaya kati ya makundi 120 yenye silaha mashariki mwa DRC.

Limekuwa likishutumiwa kufanya mauaji ya maelfu ya raia wa Congo, na kufanya mashambulizi ya bomu katika taifa la jirani la Uganda.

Kapteni Mualushayi amesema vikosi vya Congo vimewauwa wapiganaji wawili wa ADF ambao sasa wanadhibiti eneo la Bulungo linalo pakana na taifa la Uganda.

XS
SM
MD
LG