DRC : Wanamgambo wa ADF wawakata vichwa watu 16, Beni

Beni, DRC

Wanamgambo wamewakata vichwa watu 16 katika mauaji mapya kwenye kijiji kimoja karibu na Beni kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, vyanzo vya usalama vimesema Ijumaa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa raia watatu wamejeruhiwa katika mji wa Beni kutokana na mlipuko wa kilipuzi Alhamisi usiku afisa mmoja amesema, ikiwa ni dalili kuwa hizi ni mbinu mpya katika eneo hilo kutokana na ghasia za wanamgambo.

Wanamgambo wa ADF

Mauaji ya Alhamisi katika mkoa wa Mbau kaskazini mwa Beni yanashukiwa kufanya na kundi la waasi la Allied Democratic Force, ADF, ambalo linahusika na mfululizo wa mauaji tangu kuanza kwa ghasia mwezi November.

“Miili ya watu 16 waliokatwa vichwa imegundulika katika msako ulioanza jana jioni,” Jamal Moussa, msemaji wa mtandao wa taasisi za jamii za kiraia huko Mbau ameiambia AFP. Mauaji hayo yalilenga kijiji kidogo cha Mantumbi.

“Magaidi wa ADF walifanya shambulizi Alhamisi mchana, kwanza katika msitu ambako watu walikuwa katikamashamba yao, na halafu waliingia kijijini,” amesema Moussa.

Majeshi ya DRC yameanzisha operesheni dhidi ya ADF katika eneo la mashariki tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba. Lakini majibu ya ADF yamekuwa ni kufanya mauaji ya watu wengi, katika juhudi za kuwakatisha tamaa raia kulisaidia jeshi la serikali.

Kiasi cha watu 100 wameuawa tangu Novemba 5 katika mashambulizi ambayo ADF inalaumiwa kuhusika, kundi ambalo lina mizizi yake nchini Uganda.

Hakuna chanzo cha jeshi ambacho kimethibitisha rasmi ripoti ya Alhamisi lakini jeshi la Congo na lile la Umoja wa Mataifa yaliyoko katika eneo hilo yametangaza operesheni ya pamoja dhidi ya wanamgambo wa ADF katika mkoa wa Beni.

Tamko la Lucha

Kundi la kijamii la Lucha, limerioti kuwa watu tisa ndiyo wameuawa karibu na Mbau.

Abiria wawili waliokuwa katika pikipiki walirusha kilipuzi ambacho kiliripuka kwenye eneo la soko, nakujeruhi watu watatu, amesema Alois Mbwarara, mkuu wa utawala wa Rwenzori, moja ya wilaya nne katika mji huo.

ADf imekuwa ikilikimbia jeshila Congo, hivi sasa wanatumia vibaraka mjini humo kufanya vitendo vya njama,” amesema na kuongezea jeshi linafanya uchunguzi mabaki ya vifusi kubaini iwapo ni bomu la kutengenezwa nyumbani oa gruneti la mkono.

Mara ya mwisho kilipuzi kutumika huko Beni ilikuwa mwaka 2007, afisa huyo ameongezea.

Jeshi la Congo limegundua ‘kiwanda cha kutengeneza mabomu ya kienyeji’ katika kambi moja ya ADF waliyoiteka, msemaji wa jeshi jenerali Leon Richard Kasonga amesema Jumatano.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Khadija Riyami, Washington, DC.