Rais wa Marekani Joe Biden na Makamu Rais Kamala Harris wameweka mkazo mkubwa siku yao ya kwanza kamili ofisini juu ya majibu ya serikali kuu katika kupambana na virusi vya corona.
Biden alitarajiwa kuzungumza Alhamisi juu ya mipango ya utawala wake na kutia saini maagizo ya kiutendaji na hatua nyingine zinazo husiana na kupambana na COVID-19.
Wote Biden na Harris wanatarajia kuarifiwa na timu yao ya kupambana na Corona, ikiwa ni pamoja na kupata habari kuhusu hali ya sasa ya mipango ya chanjo inayo fanyika kote nchini.
Biden aliweka lengo la kuongeza chanjo mwanzoni mwa kipindi cha utawala wake ili kutoa chanjo milioni 100 katika siku 100 za kwanza.