Makamu wa Rais wa China Han Zheng, amefanya mazungumzo na Prince Mohammed Bin Salman wa Saudi Arabia mjini Beijing, China, Ijumaa.
Mohammed ambaye ni mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia Salman, aliongoza mkutano kuhusu ushirikiano kati ya China na Saudi Arabia.
Viongozi hao wawili watashiriki kusaini na kushuhudia utiaji saini wa mikataba mengine kadhaa utakaoimarisha ushirikiano kati ya nchi zao.
Vyanzo vya habari vinasema Saudi Arabia inapanga kusaini mikataba ya awali ya kuwekeza katika viwanda viwili vya kusafisha mafuta na viwanda vya madawa nchini China.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.