Changamoto zinazoukabili ushirikiano baina ya Marekani na Korea Kusini

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol (kulia) na mkewe Kim Keon-hee (kushoto) wakipanda ndege kuelekea Washington, tarehe 24 Aprili 2023. Picha na YONHAP / AFP.

Rais wa Merekani Joe Biden atamkaribisha Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol huko White House siku ya Jumatano.

Ziara hiyo ya kiserikali inaashiria uhusiano imara kati ya Marekani na Korea Kusini, ambayo mwaka huu inaadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwake. Lakini washirika hao pia wanakabiliwa na changamoto ambazo hazikutarajiwa.
Kwa njia moja au nyingine, inaonekana kama hadithi zilizopita - Korea Kaskazini kufanya uchokozi, kama ule wa kurusha kombora mapema mwezi huu.

Katika majibu yao Marekani na Korea Kusini walifanya maonyesho makubwa ya nguvu za kijeshi, kama mazoezi yale ya ndege za kivita za marekani.

Inawezekana swali kubwa zaidi ni endapo Wakorea Kusini wanaiamini Marekani kuitetea nchi yao.

Wakati Korea Kaskazini sasa inaweweza kutoa vitisho kwa Marekani, maswali mengi yamehoji endapo Washington ingeingilia kati mzozo huo.

Swali hilo muhimu ni kwa Yoon Suk Yeol mwenye mashaka na Korea Kusini ya utengenezaji wake wa silaha za nyuklia na endapo masuala yake ya kiusalama hayatashughulikiwa.

Kuwahakikishia Wakorea Kusini, Washington imetuma vifaa vyake vya kijeshi vyenye nguvu zaidi. Lakini Seoul inataka zaidi, anasema mchambuzi wa kituo cha Stimson Jenny Town.

Chanzo kingine cha mvutano ni kusita kwa Korea Kusini kuipatia Ukraine silaha. Ingawa Korea Kusini imekuwa muuzaji mkubwa wa silaha nje, inasema haiwezi kuipatia Ukraine silaha moja kwa moja kwa sababu ya sheria za nchi hiyo.

Badala yake, Korea Kusini imesaidia kwa njia isiyo ya moja kwa moja - kwa kuidhinisha uuzaji wa silaha, kama ule wa vifaru, kwa nchi kama vile Poland ambazo zinaipatia Ukraine silaha.

Mivutano kati ya Marekani na Korea Kusini kuhusu Ukraine ilifichuliwa katika uvujaji wa nyaraka za Marekani hivi karibuni , ambazo zilisema Washington ilikuwa ikiwafanyia ujasusi maafisa wakuu wa serikali wa Korea Kusini.

Seoul imepuuza tukio hilo la ujasusi, lakini Wakorea wengi bado wamekasirishwa, anasema mwanazuoni Park Won-gon wa Chuo kikuu cha Ewha.

Lakini akiwa mjini Washington, Yoon anatarajia kukutana na hadhira itakayomshangilia, wakati akiadhimisha miongo saba ya muungano huo ambao ni maarufu sana katika nchi zote mbili.