Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:27

Korea Kusini yafunguka kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na Seoul


Majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini
Majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini

Korea Kusini imetoa ripoti ya aina yake jinsi  Korea Kaskazini inavyo watendea raia wake, ikiashiria Seoul haitaendelea kuamini kwamba kukaa kimya juu ya ukiukaji wa haki kutarahisisha kusonga mbele  katika mashauriano ya kusitisha mipango ya Pyongyang ya kuboresha silaha za nyuklia na makombora.

Wizara ya Muungano (MOU), ambayo inashughulikia masuala ya ndani ya Korea, imetoa ripoti ikielezea kwa kina ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na Pyongyang kulingana na ushahidi kutoka kwa zaidi ya raia 500 wa Korea Kaskazini waliokimbilia Korea Kusini kati yam waka 2017 na 2022.

Ripoti hiyo inasema kuwa utawala wa Korea Kaskazini unawanyima wananchi wake haki ya msingi wanaposhtakiwa, kukusanyika, kujielezea na kwenda wanakotaka, kati ya mambo mengine.

Ripoti hiyo pia inasema utawala huo unapuuza thamani ya maisha ya binadamu kwa kutekeleza mauaji ya hadharani kwa watoto na watu wazima na kuwatumia watu kwa majaribio ya kimatibabu.

Ripoti hiyo yenye kurasa zaidi ya 400 iliyotolewa Machi 30 imekuja baada ya Seoul kuwa mdhamini mwenza na Umoja wa Mataifa wa rasimu ya azimio la kulaani rekodi ya ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na Korea Kaskazini iliyowasilishwa katika Baraza la Haki za Binadamu la UN Machi 21.

UNHRC ilipitisha azimio la mwaka huu siku ya Jumanne katika mkutano huko Geneva.

UN ilipitisha azimio kama hilo kila mwaka tangu 2003, lakini chini ya Moon Jae-in, ambaye alihudumu kama rais wa Korea Kusini kutoka 2017 hadi 2022, Seoul ilikataa kudhamini azimio lolote.

XS
SM
MD
LG