Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:17
VOA Direct Packages

Korea Kaskazini yarusha kombora la masafa marefu karibu na ufukwe wake wa mashariki


Silaha ya majarbio ya Korea kaskazini kwenye picha ya maktaba.
Silaha ya majarbio ya Korea kaskazini kwenye picha ya maktaba.

Korea kusini na Japan zimesema Jumamosi kwamba Korea kaskazini imerusha kombora la masafa marefu karibu na ufukwe wake wa mashariki, likiwa la pili la kichokozi mwaka huu.

Kulingana na mkuu wa jeshi la Korea kusini, silaha hiyo inakisiwa kurushwa kutokea eneo la Sunan karibu na mji mkuu wa Pyongyang saa 11 na dakika 22 za jioni kwa saa za huko.

Jeshi linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini muundo, kasi pamoja na umbali uliosafiri. Wizara ya ulinzi ya Japan imeitaja silaha hiyo kuwa aina ya ICBM, iliyochukua zaidi ya saa moja angani kabla ya kuanguka kilomita 200 magharibi mwa kisiwa cha Oshima kilichoko Hokkaido.

Hatua hiyo imefuatia onyo lililotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Korea kaskazini dhidi ya mpango wa Marekani wa kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Korea kusini kwamba yangeitumbukiza Peninsula ya Korea kwenye hali ya taharuki.

Alhamisi iliyopita, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano wa faragha mjini New York, kujadili mwenendo wa Korea kaskazini pamoja na udhibiti wa silaha, kwa mujibu wa taarifa kwenye mtandao wake.

XS
SM
MD
LG