Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:25

Korea Kaskazini yarusha makombora ya balistiki kuelekea baharini, Seoul imeripoti


Moja ya silaha za nyuklia zinazojaribiwa na Korea Kaskazini.
Moja ya silaha za nyuklia zinazojaribiwa na Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini Alhamisi ilirusha makombora ya balistiki ya masafa mafupi kuelekea kwenye  eneo la majini nje ya pwani yake ya magharibi, jeshi la Korea Kusini lilisema.

Urushaji huo umetokea wakati Marekani na Korea Kusini wakijiandaa kufanya mazoezi makubwa ya mafunzo ya kijeshi yanayofanyika baada ya miaka mingi wiki ijayo kukabiliana na tishio la silaha za nyuklia za Korea Kaskazini, ambapo kiongozi Kim Jong Un ameongeza uchokozi wake katika miaka ya karibuni licha ya nchi yake kuzidi kutengwa kiuchumi na matatizo yanayohusiana na janga la COVID-19.

Wakuu wa Wamajeshi ya Pamoja wa Kusini walisema kombora hilo lilirushwa majira ya saa kumi na mbili na dakika ishirini jioni kutoka eneo karibu na mji wa mwambao wa magharibi wa Nampo. Hakuna tathmini ya mara moja kufahamu umbali gani kombora hilo lilisafiri au wapi lilitua.

Jeshi la Korea Kusini liliimarisha mifumo yake ya upelelezi kwa harakati za Korea Kaskazini wakati ikiendelea “kujiandaa kikamilifu” kwa uratibu wa karibu na mshirika wake, Marekani, Wakuu wa Wamajeshi ya Pamoja walisema.

Kamandi ya kijeshi ya Marekani ya Indo Pacific ilisema ufyatuaji huo haukuleta “hatari ya moja kwa moja kwa majeshi ya Marekani au eneo, au kwa washirika wetu” lakini bado ilionyesha athari za silaha za nyuklia na programu ya makombora zinaletwa na hujuma ya Korea Kaskazini.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

XS
SM
MD
LG