Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:53

Rais Biden atakuwa mwenyeji wa Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Msemaji wa White House Karine Jean-Piere aliwaambia waandishi wa habari Jumanne kwamba ziara ya Rais Yoon itasheherekea maadhimisho ya miaka 70 ya ushirika wa usalama kati ya Marekani na Korea Kusini

Rais wa Marekani Joe Biden atakuwa mwenyeji wa kiongozi mwenzake wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol kwa ziara ya kikazi hapo April 26. Msemaji wa White House Karine Jean-Piere aliwaambia waandishi wa habari Jumanne kwamba ziara ya Rais Yoon itasheherekea maadhimisho ya miaka 70 ya ushirika wa usalama kati ya Marekani na Korea Kusini.

Muungano huo uliundwa baada ya vita vya miaka mitatu vya Korea ambavyo vilimalizika kwa mwaka 1953 viliiacha peninsula ya Korea ikiwa imegawanyika kati ya Kaskazini inayoongozwa na wakomunisti na Kusini inayoendeshwa kidemokrasia.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Rais Biden za kujenga na kudumisha uhusiano na washirika wa kikanda kama njia ya kukabiliana na kuongezeka kwa uwepo wa kijeshi na kiuchumi wa China pamoja na Korea Kaskazini kuendelea na program ya nyuklia na makombora ya masafa marefu licha ya vikwazo kadhaa vya Umoja wa Mataifa.

Ziara ya Yoon itakuwa ziara ya kwanza rasmi ya kiongozi wa Korea Kusini tangu mwaka 2011 wakati rais wa wakati huo Barack Obama alipomkaribisha Lee Myung-bak. Pia itakuwa ziara ya pili ya kiserikali kwa Biden tangu awe mwenyeji wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Disemba mwaka 2022.

XS
SM
MD
LG