Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:23

Korea Kaskazini yadai kuzindua kombora jipya


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un (wa pili kulia) akiwa na dada yake Kim Yo Jong (kulia), mkewe Ri Sol Ju. (2nd kushoto) na binti yake wanadhaniwa kuwa Ju Ae wakifuatilia jaribio la urushwaji wa kombora jipya la Hwasongpho-18 ICBM. Picha na KCNA KUPITIA KNS / AFP.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un (wa pili kulia) akiwa na dada yake Kim Yo Jong (kulia), mkewe Ri Sol Ju. (2nd kushoto) na binti yake wanadhaniwa kuwa Ju Ae wakifuatilia jaribio la urushwaji wa kombora jipya la Hwasongpho-18 ICBM. Picha na KCNA KUPITIA KNS / AFP.

Korea Kaskazini ilisema imefanyia majaribio kombora jipya la masafa marefu la balistiki lilonatumia mafuta imara - madai ambayo, ikiwa yatathibitishwa, huenda yakaipa Pyongyang uwezo wa kurusha makombora yasiyotabirika kwa haraka zaidi yakiilenga Marekani.

Shirika rasmi la Habari la Korea Kaskazini lilisema kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un alisimamia uzinduzi wa kombora la Hwasong-18 siku ya Alhamisi, ambapo alisema litaboresha kwa kiasi kikubwa mkakati wa nchi hiyo kudhibiti na kukabiliana na mashambulizi ya nyuklia.

Kim "alielezea kuridhishwa kwa kiasi kikubwa kuhusu mafanikio ya ajabu" ya majaribio hayo, shirika la habari la KCNA liliripoti, na kuongeza kuwa maadui wa nchi hiyo sasa "wana wasiwasi na hofu kubwa ... kwa hivyo wanajuta kwa uchaguzi wao mbaya wa kukata tamaa."

Korea Kaskazini kwa muda mrefu imekuwa ikitaka kutengeneza makombora ya ICBM yanayotumia nishati maalum, ambayo kwa nadharia ni vigumu sana kwa maadui zake kama Marekani kugundua na kujaribu kuzuia.

Kabla ya hapo, ICBM zote tatu za Korea Kaskazini zimefanyiwa majaribio yakitumia mafuta ya kioevu , ambayo ni lazima yajazwe kwenye roketi katika mchakato ambao unaweza kuchukua masaa mengi na kuhitaji vifaa vya kisasa vinavyoonekana kirahisi kutoka angani.

Hata hivyo roketi zinazotumia makaa, huwashwa kabla. Makaa pia ni thabiti zaidi, na kuyafanya makombora kama haya kuwa rahisi kusonga katika mazingira hatari ya vita.

Picha za vyombo vya habari vya serikali zilimuonyesha kiongozi huyo wa Korea ya Kaskazini, Kim akiwa ameshikana mikono na binti yake mdogo, wakitazama kombora hilo likiibuka kutoka kwenye moshi mwembamba wenye rangi ya chungwa.

Shirika la habari la KCNA lilitoa maelezo machache ya kiufundi kuhusiana na kombora hilo jipya, ikiwemo upeo wake wa juu zaidi ulionao.

Katika taarifa iliyotolewa na jeshi la Korea Kusini lililitaja jaribio hilo kuwa ni kama la awali, na kuongeza kuwa "muda na juhudi zaidi" zinahitajika ili kuyamudu makombora mapya ya masafa marefu, unaoendeshwa na mfumo wa makaa.

XS
SM
MD
LG