Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:17
VOA Direct Packages

Mwanamuziki maarufu wa K-Pop afariki dunia kwake nyumbani mjini Seoul


Mwanamuziki wa kundi la K-Pop la ASTRO, Moon Bin,aliyefariki akiwa kwake nyumbani mjini Seoul
Mwanamuziki wa kundi la K-Pop la ASTRO, Moon Bin,aliyefariki akiwa kwake nyumbani mjini Seoul

Moon Bin muimbaji  wa bendi maarufu ya wanaume ya Astro ya Korea Kusini, amepatikana akiwa amekufa ndani ya nyumba yake mjini Seoul, kulingana na wasaidizi wake.

Ripoti za kifo cha Bin mwenye umri wa miaka 25 zimetolewa na meneja wake baada ya kufika nyumbani kwake Jumatano jioni kutokana na mwanamuziki huyo kutojibu simu kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap, polisi wanachunguza sababu ya kifo, ingawa hakionyeshi dalili kwamba aliuwawa.

Timu ya wasaidizi wake ijulikanayo kama Fantiago imethibitisha kifo hicho Alhamisi, kupitia taarifa, ikisema kuwa “ alituacha ghafla na alikuwa nyota mawinguni”, na kwamba wanamuziki wenzake pamoja na wafanyakazi wengine kwenye kampuni yake wanaendelea kumuomboleza kwa huzuni kubwa na mshtuko.

Fantiago imesema kwamba mazishi yake yatahusisha watu wachache iwezekanavyo, wengi wakiwa wanafamilia, wanamuziki wenzake na marafiki wa karibu. Moon Bin alianza muziki 2016 akiwa mmoja wa wanamuziki 6 wanaume kwenye bendi ya Astro, iliyoshamiri sana muda mfupi baada ya kuletwa kwenye show moja maarufu ya televisheni nchini humo.

XS
SM
MD
LG