Hatua hii iliyotangazwa na Canada imekuja wakati waasi wakionekana kusonga mbele nchini kote wakiteka miji mikubwa.
Hali nchini Afghanistan ni ya kusikitisha na Canada, haitakaa tu, Waziri anayehusika na masuala ya uhamiaji, Marco Mendicino aliuambia mkutano wa waandishi wa Habari.
Wakimbizi hao watajumuisha raia wa Afghanistan walio katika mazingira hatarishi ambao bado wako nchini humo au ambao tayari wamekimbilia mataifa Jirani.
Wakimbizi hao ni pamoja na viongozi wa kike na wafanyakazi wa serikali, pia inajumuisha watetezi wa haki za binadamu, watu wachache walioteswa na waandishi wa Habari.
Ndege kadhaa za wanaotafuta hifadhi zimeondoka na ndege ya kwanza ilitua Ijumaa huko Toronto, Mendicino alisema.