Bunge la Msumbiji laidhinisha mswaada wa kuhalalisha wanamgambo kushiriki katika vita jimbo la Cabo Delgado

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi,

Bunge la Msumbiji limeidhinisha mswaada wa sheria inayohalalisha kujihusisha kwa wanamgambo katika vita dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado.

Polisi wa Rwanda wakifanya doria katika mji wa Palma, Jimbo la Cabo Delgado, Msumbiji, Aug. 15, 2021.

Wanamgambo wa jimbo hilo wamekuwa wakisaidia jeshi na washirika wao kutoka Rwanda na Jumuia ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika katika vita dhidi ya wapiganaji wa kislamu katika jimbo hilo.

Wanajeshi wa Rwanda wakiwa katika eneo mchimbo ya mradi wa nishati la Cabo Delgado, Msumbiji.

Waziri wa ulinzi Cristovao Chume aliyewasilisha mswaada huo bungeni amekiri kwamba jeshi la msumbiji halina uwezo wakutosha kupambana pekee yao na harakati za wapiganaji wa Kiislamu.

Anasema kuna haja ya dharura kubuni kikosi cha jimbo ili kuimarisha jeshi kuweza kupambana na kudhibiti kuenea kwa mashambulizi ya wapiganaji.