Hali ya dharura iliyowekwa na Rais Felix Tshisekedi Mei 06, imeongezewa muda mara sita sasa.
Kati ya wabunge 335, waliopiga kura kuunga mkono uamuzi huo ni 334, wakati mmoja hakupiga kura.
Utawala wa kijeshi umechukua nafasi za utawala wa kiraia ili kuzuiya hali ya kutokuwa na usalama katika majimbo ambako mashambulizi kadhaa yamefanywa na waasi na kusababisha maelfu ya vifo vya watu.
Ghasia zimeongezeka licha ya kuwepo maelfu ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa.
Baadhi ya mashambulizi yamelaumiwa kufanywa na majeshi ya ADF, zaidi ya darzeni za makundi yenye silaha yanafanya operesheni zake huko.
Majimbo ya mashariki pia yameshuhudia ghasia baina ya makundi ya kikabila.