Mkutano huo umefanyika wakati muhimu Ulaya baada ya Russia kuweka wanajeshi 100,000 karibu na mpaka na Ukraine.
Mkutano huo pia umefanyika baada ya mazungumzo mapana kati ya Moscow na nchi za magharibi wiki iliyopita kushindwa kutatua maswala yenye utata kuhusu Ukraine, na mambo mengine ya usalama.
Blinken anatarajiwa kukutana na Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergey Lavrov mjini Geneva, kesho Ijumaa.
Amewasili Ujerumani baada ya kuitembelea Ukraine ambapo alikutana na rais Volodymyr Zelenskyy na kumuahidi msaada wa Marekani.
Marekani imesema kwamba itatoa msaada wa ziada wa kiasi cha dola milioni 200 kwa Ukraine, kwa ajili ya ulinzi wa kijeshi.