Baraza la Wawakilishi lachambua Trump kutochukua hatua kwa zaidi ya saa tatu

Mwenyekiti Bennie Thompson, D-Miss., na Makamu wake Liz Cheney, R-Wyo., wa Jopo linalochunguza uvamizi wa Jan. 6 katika Bunge la Marekani wakitoa ushahidi wakitaka Rais wa zamani Donald Trump afunguliwe mashtaka ya kulidhalilisha Bunge, Washington, Dec. 14, 2021. (AP Photo/J. So

Mwenyekiti Bennie Thompson, D-Miss., na Makamu wake Liz Cheney, R-Wyo., wa Jopo linalochunguza uvamizi wa Jan. 6 katika Bunge la Marekani wakitoa ushahidi wakitaka Rais wa zamani Donald Trump afunguliwe mashtaka ya kulidhalilisha Bunge, Washington, Dec. 14, 2021. (AP Photo/J. So

Uchunguzi wa Baraza la Wawakilishi la Marekani katika ghasia zilizofanyika katika jengo la Bunge la Marekani Januari mwaka jana unachambua kwa nini wakati huo - Rais Donald Trump hakuchukua hatua kwa zaidi ya saa tatu.

Trump hakuchukua hatua kuwazuia wafuasi wake kushambulia jengo hilo na kupambana na polisi wakati wabunge wakishughulika kuthibitisha kuwa alikuwa ameshindwa uchaguzi wa 2020, mwenyekiti wa jopo hilo amesema Jumapili.

Mwakilishi Bennie Thompson wa Mississipi amekiambia kipindi cha “State of the Union” cha CNN kuwa jopo hilo la wachunguzi lenye wajumbe tisa linataka kujua Trump alikuwa anafanya nini “katika dakika 187 za kutochukua hatua yoyote,” alipokuwa akiangalia machafuko yakiendelea kutokea kupitia televisheni kutoka chumba cha chakula mbali na ofisi ya Oval huko White House.

“Tulikaribia sana kupoteza demokrasia yetu,” Thompson amekosoa.

Mmoja wa wanakamati wawili Warepublikan, Mwakilishi Liz Cheney wa Wyoming, mkosoaji mkuu wa Trump, amekiambia ktiuo cha televisheni cha ABC katika kipindi cha “This Week”, angeweza kuwaambia [Wafanya ghasia] kuacha hilo. Hakufanya hivyo.”

Thompson amesema, “Rais ameenda mahakamani kujaribu kutuzuia kuona rekodi” za mazungumzo yake ya simu, ujumbe mwingine na nyaraka wakati binti yake Ivanka Trump, wabunge wa Republikan na maafisa wa utawala wa Trump walimtaka kutoa tamko kuwataka zaidi ya wafuasi wake 800 waliokuwa ndani ya Bunge kuondoka eneo hilo.

“Kile ambacho anakifanya ni mwenendo wa kawaida wa Donald Trump,” Thompson amesema. “Anafungua mashtaka, anakwenda mahakamani, anajaribu kuchelewesha mambo. Lakini tunaamini tutaweza kupata haki ya kusikiliza mazungumzo yake ya dakika 187.

Mahakama ya rufaa ya Marekani mjini Washington imetoa uamuzi kuwa kamati ya uchunguzi ina maslahi muhimu ya kipekee” katika kuona nyaraka zozote zinazohusiana na vurugu hizo na mipango yake, lakini Trump amekata rufaa Mahakama ya Juu kubatilisha uamuzi wa mahakama ya chini, akisema nyaraka zake za White House zililindwe kuufikia umma.

Katika mkusanyiko karibu na White House kabla ya Januari 6, 2021, ghasia kutokea, Trump aliwataka wafuasi wake “kupigana kwa nguvu zote” katika Bunge hilo ili kuwazuia wabunge kuthibitisha kuwa Mdemokrat Joe Biden alikuwa amemshinda kwenye uchaguzi wa Novemba 2020. Zaidi ya watu 725 waliokuwa wameshiriki katika ghasia wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya aina mbalimbali ya uhalifu, ikiwa ni makosa madogo ya kukiuka amri ya kutoingia bungeni hadi makosa makubwa ya uhalifu, ikiwemo kuwashambulia polisi.

USA, Washington, Picha za ghasia zilizotokea Bunge la Marekani.

Wakati akipuuza ushauri wa awali ukimtaka atoe amri ya waandamanaji kutawanyika, Trump hatimaye alitoa video fupi akiwataka wafanya fujo kuondoka, lakini akiwaambia, “Tunawapenda; nyinyi ni watu adhimu kwetu.”

Kama afanyavyo hadi hivi leo, Trump alisema katika video nadharia za hujuma za uongo kuwa yeye ndiyo kweli aliyeshinda uchaguzi, akisema, “Nafahamu maumivu yenu; najua mmeumia. Tulikuwa na ushindi wa uchaguzi ulioibiwa kutoka kwetu. Ilikuwa ni ushindi wa kishindo na kila mmoja anajua hili. Hususan upande wa pili. Lakini lazima muende nyumbani hivi sasa. Ni lazima tuwe na amani.”

Baada ya waandamanaji kuondolewa hatimaye katika majengo ya Bunge, Baraza la Wawakilishi lilimthibitisha Biden kuwa mshindi wa uchaguzi katika saa za awali Januari 7.