Seneta Chuck Grassley, Mrepublican anasema:“Miaka yako nane na ujuzi wa awali kama mwanasheria mkuu wa Florida kwa miaka minane, inakutayarisha, ninauwezo wa kuifanya kazi hii kwa ufanisi.”
Trump amemchagua Seneta Mrepublican Marco Rubio kuwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani, na anatarajiwa kuidhinishwa…….
Seneta Marco Rubio, Chaguo la kuwa Waziri wa Mambo ya Nje anaeleza: “Rais anapanga sera za mambo ya nje – kazi yetu katika Wizara itakuwa kutekeleza.”
Lakini Pete Hegseth, aliyetajwa na Trump kuongoza Pentagon, hajawahi kushika nafasi ya uongozi katika jeshi. Alikuwa akiongoza kipindi katika kituo cha televisheni cha Fox News.
Pete Hegseth, Chaguo la Waziri wa Ulinzi anasema: “Tunaweka wapiganaji vita kwanza. Ndicho Donald Trump amenieleza nikifanye. Kazi yao ni kurudisha maadili ya vita kwenye Pentagon.”
Hegseth ni mmoja wa wale waliotajwa mwenye historia ya matamshi yenye utatanishi ambapo baadhi ya maseneta wa Republican huenda watakuwa na wakati mgumu kumthibitisha.
Shannon O’Brien, Chuo Kikuu cha Texas amesema: “Rais ajaye Trump hana haja ya kufikiria kuwa wataanguka. Kwasababu huenda baadhi yao wako upande wa Republican, kama hawatapewa fursa au heshima yao, wanaweza kufanya maisha yake kuwa magumu sana.”
Kiongozi wa walio wengi ajaye, Mrepublcian John Thune, ameahidi kuitisha upigaji wa haraka kwa wale Trump aliowataja kuwapa wadhifa.
Seneta John Thune, Mrepublican anaeleza: “Tutafanya kila kitu tunachoweza ili mchakato wa uteuzi uende haraka, tunataka waingie katika nafasi zao ili tuweze kutekeleza ajenda zake.”
Lakini Trump amependekeza aliowataja kushika nafasi za uwaziri ufanyike wakati baraza la Seneti liko katika mapumziko, mara nyingine ni mpango wa kuachana na jukumu la kikatiba la wabunge la kuwaidhinisha wateuliwa.
Shannon O’Brien, Chuo Kikuu cha Texas amesema: “Je kama rais atajaribu kwa makusudi kuakhiria Bunge, atumie madaraka yake ili afanye uteuzi wakati bunge likiwa likizo? Hilo halijawahi kutokea. Lakini anaposema anataka wafanye hivyo, njia pekee ambayo huenda akalazimisha hilo itakuwa ni kuakhirisha Bunge. Hilo linaweza kuishia mahakamani.”
Maseneta wa Republican tayari wanajibu hilo.
Seneta John Cornyn, Mrepublican anaeleza: “Ndiyo, hilo ni suala jingine. Kwa hakika, sidhani tuntakiwa tuachane na majukumu ya Seneti.”
Marais wa Marekani kutoka vyama vyote viwili wamefanya uteuzi wakati bunge likiwa likizo. Lakini Mahakama ya Juu iliweka kiwango wakati wa awamu ya uongozi wa Rais Barack Obama.