Baadhi ya Wakenya na raia wa kigeni waondoka nchini kabla ya uchaguzi

Willian Ruto na Raila Odinga

Mamia ya raia wa Kenya na wageni, ambao wamekuwepo nchini Kenya, wameondoka na  kuelekea Uganda kupitia mipaka ya Busia na Malaba kabla ya uchaguzi wa urais wenye ushindani mkali kufanyika Agosti 09.

Wakati wagombea wanne wako katika kinyang’anyiro cha nafasi ya juu ya uongozi Kenya, ushindani ni mkali kati ya mgombea wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) William Ruto na Raila Amollo Odinga wa chama cha Azimio la Umoja.

Wageni wanaowasili nchini Uganda kutoka Kenya ni pamoja na Warundi, Wanyarwanda, Waasia, raia wa Marekani, na Uingereza ambao wameliambia gazeti la Monitor kuwa wanahofia kutokea tena kwa ghasia za baada ya uchaguzi kama zile za mwaka 2007 ambazo ziliitikisa Kenya.

Wakati wa ghasia hizo, zaidi ya watu 10 waliuawa, mamia walijeruhiwa na maelfu kukoseshwa makazi.

“Ghasia hizo bado zinakumbukwa na Wakenya wengi katika fikra zao. Ndiyo sababu watu wanajaribu kuondoka nchini kabla ya uchaguzi,” raia wa Kenya Mr Ramadan Otyeno alisema Jumatatu.

Baadhi ya sehemu za Kenya zimekuwa chini ya amri ya kutotoka nje na kuna masharti ya kutoka na mikusanyiko ya usiku kabla ya uchaguzi utakao amua rais wa tano wa taifa hilo.

Bw Ssebbo Ogongo, raia wa Uganda, ambaye amekuwa akiishi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, kwa miaka kadhaa, Jumamosi usiku alichukua vitu vyake vingi anavyomiliki katika lori kurejea nyumbani.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la Monitor linalochapishwa Uganda.