Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:59

Rais Kenyatta kuhutubia taifa


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akizungumza kwa njia ya video.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akizungumza kwa njia ya video.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alitarajiwa  kutoa hotuba yake ya mwisho kwa wakazi wa Mlima Kenya katika mahojiano ambayo yatarushwa kwenye vituo vyote vya redio nchini humo kutoka eneo hilo.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alitarajiwa kutoa hotuba yake ya mwisho kwa wakazi wa Mlima Kenya katika mahojiano ambayo yatarushwa kwenye vituo vyote vya redio nchini humo kutoka eneo hilo.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation ingawa maudhui ya mahojiano yake hayajafichuliwa, mahojiano hayo yanayofanyika chini ya saa 48 kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9 na yametajwa kuwa shambulio lake la mwisho dhidi ya Naibu wake William Ruto ambaye amekuwa akifanya kampeni dhidi yake.

Baadhi ya wakosoaji wake wameifahamisha moja kwa moja Tume ya Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kupitia mitandao ya kijamii kwamba Rais Kenyatta ananuia kukiuka matakwa ya chombo hicho kwamba wagombea na vyama vya siasa waache kujihusisha na vitendo vyovyote vya kampeni za kisiasa saa 48 kabla ya uchaguzi

Hata hivyo, Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alipokuwa akihutubia wanahabari katika ukumbi wa Bomas of Kenya alisema kuwa Rais Kenyatta si mgombea na yuko huru kutoa hotuba zake au matangazo yoyote.

Kipindi rasmi cha kampeni kilianza Juni 7 baada ya IEBC kukamilisha shughuli ya usajili wa wagombea na kukamilika Jumamosi saa kumi na mbili jioni.

IEBC katika taarifa yake ilisema yeyote atakayebainika kukiuka masharti haya atatajwa kuwa amekiuka Kanuni za Maadili ya Uchaguzi.

Rais Kenyatta hata hivyo, si mgombea katika uchaguzi wa mwaka huu.

XS
SM
MD
LG