Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 22:17

Mamlaka Uganda zachukua tahadhari kipindi cha mpito wa uchaguzi Kenya


Wagombea Urais uchaguzi mkuu Kenya 2022, Willian Ruto and Raila Odinga.
Wagombea Urais uchaguzi mkuu Kenya 2022, Willian Ruto and Raila Odinga.

Mamlaka nchini Uganda zimewataka wafanyabiashara kujiweka sawa kukabiliana na “wiki ngumu” wakati Kenya, ambayo ndio njia kuu ya kusafirisha bidhaa, inafanya uchaguzi.

Wakati hakuna ushahidi wa kuaminika wa tishio la usalama ambalo linaweza kuvuruga operesheni za usafirishaji katika njia ya kaskazini maarufu kama “Northern Corridor”, wafanyabiashara wameshauriwa kuchukua tahadhari, ama kwa kuchelewesha uagizaji bidhaa au kutumia njia mbadala ya kati “Central Corridor”.

Uganda pia imewashauri raia wake wanaoishi na kufanya kazi nchini Kenya kuchukua tahadhari, baada ya Marekani kutoa ilani ya kusafiri kwa wale wanaotembelea mji wa Kisumu.

Hili limekuja wakati Rais Uhuru Kenyatta na maafisa wake wameihakikishia kanda nzima kuwa uchaguzi utakuwa wa amani. Na hata wagombea wa juu wa urais William Ruto na Raila Odinga wameahidi amani – na kukubali kushindwa iwapo upigaji kura utakuwa huru na wa haki.

Wakati akihutubia Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Arusha mwezi uliopita, Rais Kenyatta alisema kuwa hakuna kitakacho haribika.

Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang’i pia amesema vyombo vya usalama vimeimarishwa kuhakikisha usalama katika uchaguzi na nchi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Henry Okello Oryem alisema anatarajia uchaguzi utamalizika kwa salama lakini Uganda ilikuwa inajiandaa na hali yoyote yenye itakayojitokeza ikiwa na mpango B wa kuwa na akiba ya bidhaa muhimu na kubadilisha njia usafarishaji bidhaa kup Tanzania.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la “The East African” linalochapishwa nchini Kenya

XS
SM
MD
LG