Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:26

Maafisa wanne wa kusimamia uchaguzi wafukuzwa kazi Kenya

Maandalizi ya vifaa vya kupiga kura uchaguzi mkuu Kenya 2022.
Maandalizi ya vifaa vya kupiga kura uchaguzi mkuu Kenya 2022.

Maafisa wanne wa Tume ya Uchaguzi, ambao waligundulika  wanafanya mkutano katika nyumba ya aliyekuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la kaunti (MCA) ambaye ni mgombea wa Homa Bay, magharibi mwa Kenya, wamefukuzwa kazi.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) iliwaondoa kazini kwa kutenda makosa ya uchaguzi.

Afisa wa IEBC anayesimamia uchaguzi Kaunti ya Homa Bay Fredrick Apopa alisema maafisa walifanya makosa kuhudhuria mkutano huo.

“Huwezi kuwa katika mkutano na wanasiasa wakati sheria inakutaka usiegemee upande wowote,” alisema.

Bw Apopa alisema maafisa waliripotiwa walikuwa wakikutana na MCA na mgombea ubunge kutoka chama cha kisiasa, kati ya watu wengine.

Haikujulikana nini kikundi hicho kilikuwa kinajadili.

Lakini wakazi wa Kanyikela ambao waliuvamia mkutano huo na kuwachukua washukiwa wa kosa hili kwenda kituo cha polisi walidai walikuwa wanapanga namna ya kughushi uchaguzi wa Jumanne.

Bw Apopa alisema wachunguzi wanatathmini madai hayo na watachukuwa hatua za lazima iwapo washukiwa hao watabainika wamefanya kosa la kiuchaguzi.

Baadhi ya watu waliohojiwa ni wakazi ambao waliwakamata washukiwa hao na kuwapeleka kituo cha polisi cha Ndhiwa.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African" linalochapishwa Kenya

XS
SM
MD
LG