Ama Naibu Rais William Ruto au kiongozi mkongwe wa upinzani na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga atakuwa rais wa tano wa Kenya.
Wawili hao wote ni wa jamii ya wanilote. Ni mara ya kwanza Kenya kwa wanaoongoza katika kinyang’anyiro cha kuingia madarakani wote ni wa jazmii ya wanilote.
Katika ngazi pana zaidi ya Afrika Mashariki, mwaka 1985 nchini Uganda, Milton Obote, ambaye alirejea madarakani kama rais katika uchaguzi uliokuwa na utata mwezi Disemba 1980, aliondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi kwa mara ya pili – mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1971 katika mapinduzi yaliyoongozwa na Field Marshal Idi Amin. Nchini Kenya, Daniel arap Moi alikuwa amezama katika siasa za utawala wa chama kimoja.
Kwa kipindi cha miaka minne na nusu Obote alikuwa madarakani, na kwa mara ya kwanza kulikuwa na viongozi wa jamii wa wanilote madarakani Afrika Mashariki.
Utamaduni wa udugu umekuwa na athari ya kutosha katika siasa za kieneo na sera za mambo ya nje kwa namna ambayo mara nyingi hazizingatiwi kikamilifu. Kwa mfano, Rais Moi alimteua Jenerali Lazaro Sumbeiywo, mwakilishi maalum wa Kenya katika Mamlaka ya Muungano wa Serikali katika Maendeleo – kuongoza mchakato wa amani ya Sudan kati ya m waka 1997 na 1998.
Baadae alimteua kuwa msuluhishi katika mchakato wa amani uliofanyika Nairobi mwaka 2001.
Aliendelea kuwepo madarakani na Rais Mwai Kibaki, Jenerali Sumbeiywo alisaidia kuleta nyumbani aina fulani ya Mkataba Kamili wa Amani uliojulikana kama Naivasha Agreement Januari 9, 2005 uliokuwa kati ya wapiganaji wa Sudan People’s Liberation Movement na Serikali ya Sudan.
Mkataba huo wa Amani ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan vilivyodumu kwa miaka 25.
Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African" linalochapishwa Kenya.