AU yalaani shambulizi la kigaidi lililouwa watu zaidi ya 79 Somalia

Wafanyakazi wa Hospitali wakiwa wanampeleka mtu aliyejeruhiwa katika ndege ili anayesafirishwa kwa ndege kwenda kutibiwa Uturuki baada ya shambulio la bomu mjini Mogadishu, Somalia, Disemba. 29, 2019.

Umoja wa Afrika, AU, umelaani shambulio la kigaidi lililouwa watu wasiopungua 79 na kujeruhi wengine 149 mjini Mogadishu, Somalia Jumamosi na imesema itafanya juhudi zaidi kuimarisha usalama katika nchi ya Pembe ya Afrika.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU Moussa Faki Mahamat amesema taasisi hiyo haitapuuzia vitendo vya uhalifu kama hivyo dhidi ya ubinadamu, ikisisitiza kuwa haitatishika kwa vitendo vya uoga vya kihalifu vinavyofanywa na magaidi ambao hawataki amani iwepo Somalia.

"Kuunga mkono kwetu Serikali Kuu ya Somalia, na kazi yetu tunayotekeleza Somalia itaendelea hadi kufikia lengo lake na dhamiri yake kupitia majukumu yake na kutekeleza matakwa ya kisheria ya wananchi wa Somalia ya kuishi wakiwa huru, kwa amani na usalama, " amesema Mahamat katika tamko la vikosi vya kulinda amani vya AU nchini Somalia (Amisom) Jumapili

Mapema Jumapili mtu aliyejitoa muhanga aliripua gari katika eneo la kukagua magari lililokuwa na shughuli nyingi ambako magari kadhaa yalikuwa yamejipanga katika kupitia ukaguzi wa kiusalama nje kidogo ya mji wa Mogadishu.

Kati ya wale waliouawa katika mlipuka ni pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu, wanawake, watoto na wafanyakazi wa vikosi vya usalama wa taifa vya Somalia.