Mauaji hayo yalifanyika kabla ya watu hao kuiba silaha na kuchoma majengo, vyanzo viwili vya usalama vimesema Jumatatu.
Haikufahamika mara moja ni nani aliyefanya uvamizi wa Jumamosi huko Mutumji, lakini jeshi linahusika katika operesheni huko Zamfara dhidi ya magenge ya wahalifu wenye silaha wanaojulikana kama majambazi ambao wanalaumiwa kwa kuhusika na mfululizo wa utekaji nyara wa watu wengi.
Mawasiliano ya simu pia yamekatwa huko Zamfara na katika sehemu za jimbo jirani la Katsina katika jaribio la kuvuruga mawasiliano ya majambazi juu ya harakati za kijeshi wakati wa msako.
Waliwashinda wanajeshi na kuua 12 kati yao. Ambao ni pamoja na wanajeshi 9 wa jeshi la majini , mwanajeshi mmoja na polisi wawili. Chanzo cha pili cha usalama kilithibitisha maafa hayo.
Vyanzo vya habari hii ni mashirika la habari ya AFP/Reuters