Kwa miaka kadhaa alikuwa ni mkosoaji machachari wa Rais Vladimir Putin na sera zake, alirejea Russia baada ya kupata nafuu kutokana na shambulizi la sumu iliyokaribia kumuua ambalo wafuasi wake wanasema lilielekezwa na Kremlin. Alikamatwa mara baada ya kuwasili nchini.
Siku ya Ijumaa hakuweza kuokolewa na madaktari alipopoteza fahamu baada ya kutoka nje kutembea, idara ya magereza zilisema.
Muda wote alipokuwa jela, mpinzani huyo mwenye umri wa miaka 47 alionekana katika kanda za video zilizokuwa na chengachenga katika mahakama za muda zilizokuwa zikisikiliza kesi zake, akithubutu kumkosoa Putin kutokana na uvamizi wake huko Ukraine.
Ujumbe wake – ulitumwa kwa wafuasi wake kupitia maudhui yaliyowekwa katika mitandao ya kijamii – yakilinganisha tofauti kubwa kati yake na Putin, aliye na mtindo wa Soviet, jasusi wa zamani wa KGB mwenye umri wa miaka 71 aliyetawala kwa zaidi ya miaka 20.
“(Russia) inaogelea katika dimbwi ambalo liko ama katika matope au damu, ikiwa imevunjika, na watu wake wakiwa maskini na walionyang’anywa haki yao, ikizungukwa na maelfu ya watu waliouawa katika vita vya kijinga na visivyokuwa na maana katika karne ya 21,” Navalny alisema katika moja ya taarifa zake.
Ukosoaji wake, ambao unaendana na msimamo wa maelfu ya wafuasi wake, umethibisha kuwa ni chanzo cha kero kwa upande wa Kremlin ambapo makundi ya haki za binadamu yakiishutumu kwa kuwaangamiza wapinzani wake kwa njia yoyote inayoonekana ni muhimu.
Hivyo basi kifo chake kitaendeleza wasiwasi huu wa ukandamizaji wa wapinzani hao.
'Si ogopi'
Mwaka 2018, alikuwa amefanya kampeni nchi nzima kuwa rais, alichapisha uchunguzi wa ufisadi uliopo ulioidhalilisha Kremlin na kukusanya makundi makubwa kuandamana mitaani nchini Russia.
Kurejea kwake nchini Russia mwezi Januari 2021 licha ya kukabiliwa na kifungo ilimfanya akwaruzane na Putin, baada ya Navalny kulaumu kitendo cha kushambuliwa kwa sumu huko Siberia dhidi ya Kremlin.
“Siogopi nakutaka na wewe pia usiogope,” alisema katika wito wake kwa wafuasi wake alipokuwa anawasili Moscow, muda mfupi kabla ya kukamatwa kwa mashataka yaliyohusishwa na hukumu ya zamani ya ubadhirifu.
Kukamatwa kwake kulichochea baadhi ya maandamano makubwa sana Russia ambayo hayajawahi kuonekana kwa miongo kadhaa, na maelfu walikamatwa katika mikusanyiko hiyo nchi nzima yakimtaka aachiliwe.
Timu ya Navalny ilimkabili Putin na toleo la “Kasri ya Putin”, uchunguzi ambao unahusiana na nyumba ya kifahari huko Black Sea ambayo timu yake inadai ilitolewa zawadi kwa Putin kwa njia ya ufisadi.
Kashfa hiyo ilimlazimisha Putin kukanusha jambo ambalo ni nadra kulifanya, na kusema kuw, ingekuwa vyombo vya usalama walikuwa wanahusika hasa na shambulizi la kumpa sumu, wangekuwa wameimaliza kazi hiyo.
Wakati Navalny alikuwa anajiamini katika matumizi ya mitandao, Putin anajulikana kwa yote mawili ikiwemo kutotumia intaneti na kumuuliza kijana aliyemtaka amfuatilie katika katika mtandao wa YouTube: “Vipi niandike kuingia katika mtandao?”
Kanda kama ile ya video ya ufisadi ya Navalny ikimlenga aliyekuwa waziri mkuu Dmitry Medvedev ilichochea maandamano makubwa mwaka 2017, huku waandamanaji wakibeba bata wa bandia ambao walikuja kuwa ni alama ya maandamano hayo.
Kabla ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2018, Navalny alitembelea miji kadhaa kote nchini ili kuomba kuungwa mkono lakini alizuiliwa kushiriki katika uchaguzi kwa sababu ya mashtaka ya wizi wa zamani.
“(Putin) ananiogopa na anawaogopa watu ninao wawakilisha,” aliiambia AFP wakati huo.
Kabla ya hapo alikuwa ameshindana na Sergei Sobyanin akitaka kuwa meya wa Moscow na kusababisha uchaguzi kurudiwa.
'Wahuni na Wezi'
Katika mikutano yake ya hadhara na mahakamani, Navalny alikuwa mzungumzaji mwenye ushawishi katika mikutano ya umma na kuwakusanya waandamanaji kwa kutumia misemo maarufu kama vile “chama cha wahuni na wezi” kukosoa chama tawala cha United Russia.
Lakini amekuwa akichafuliwa na ukosoaji ndani ya misimamo ya uzalendo ya mrengo wa kulia, na kanda ya video iliunga mkono silaha iliyokuwepo tangu 2007 ikijirejea mara kwa mara ambapo aliwafananisha watu kutoka iliyokuwa Soviet kwenye mkoa wa South Cuacasus na mende.
Navalny pia aliendelea kuwa ni mtu anayonekana kwa jamii ya Russia wanaounga mkono maelezo rasmi ya Kremlin kuhusu yeye kuwa ni kibaraka wa Magharibi na mhalifu wa jinai.
Alikuja kuwa ni kero kwa Kremlin kiasi cha Putin kukataa kulitaja jina lake hadharani. Kikundi chake cha kupambana na ufisadi kilisambaratishwa, na washirika wake wa juu wako walifungwa na wengine kwenda ukimbizini.
'Huwezi kuninyamazisha'
Navalny's team said he had been harassed in prison and repeatedly moved to a punitive solitary confinement cell.
Timu ya Navalny ilisema kuwa alikuwa akibughudhiwa jela na mara kwa mara kuhamishwa na kuadhibiwa kwa kuwekwa chumba cha peke yake.
Alisema walinzi walikuwa wamewalazimisha yeye na wafungwa wengine “kuteswa kisaikolojia na Putin,” kwa kuwalazimisha kusikiliza hotuba za rais.
Licha ya hilo Navalny aliendelea kuwa mchangamfu na mdhalilishaji kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii zikihaririwa na wasaidizi wake, licha ya kuwa katika hali hiyo.
Wakili kwa taaluma alipigania haki za msingi na kuwashtaki mahakamani maafisa wa magereza. Alikuwa pia akiwashutumu, akifungua maombi rasmi kupewa ala ya muziki ya asili – kimono na balalaika – na kuruhusiwa kuweka mnyama.
“Hamuwezi kuufunga mdomo wangu,” alitangaza.