Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:12

Putin asaini sheria ya kutaifisha mali za wataopatikana na hatia ya kukashifu jeshi


Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Rais wa Russia Vladimir Putin amesaini sheria Jumatano ambayo itawawezesha maafisa wa usalama kutaifisha fedha, vitu vya thamani na rasilimali nyingine kwa watu waliokutikana na hatia ya kueneza “kwa makusudi taarifa potofu” kuhusu jeshi la nchi hiyo.

Mswaada huo ulipitishwa na mabaraza yote mawili ya Bunge la Russia, na kuthibitishwa kwa kauli moja na baraza dogo wiki iliyopita.

Spika wa baraza kubwa, Vyacheslav Volodin, alisema hatua hiyo inajumuisha adhabu kali zaidi kwa “ wasaliti ambao wanaipaka matope nchi yetu na majeshi yetu” na “kuwavua heshima walizotunukiwa hao wahuni, kuwanyang’anya mali zao, fedha na vitu vingine vya thamani.”

FILE - Vyacheslav Volodin
FILE - Vyacheslav Volodin

Maafisa wa Russia wametumia sheria zilizopo dhidi ya “wanaochafua” jeshi hilo ikiwemo makosa kama yale “yakuhalalisha ugaidi” na kueneza “habari potofu” kuhusu jeshi la ulinzi kuwanyamazisha wakosoaji wa Putin. Wanaharakati kadhaa, mabloga na raia wa kawaida wa Russia wameadhibiwa kwa kifungo cha jela cha muda mrefu.

Sheria hiyo mpya ya utaifishaji itatumika kwa wale wanaokutikana na hatia ya uchochezi wa wazi wa “harakati za siasa kali” na kuwataka watu kuchukua hatua zenye madhara kwa usalama wa taifa au”kulichafua” majeshi ya ulinzi.

Kulichafua jeshi la ulinzi la Russia limekuwa ni kosa la jinai chini ya sheria iliyopitishwa kama sehemu ya msako wa jumla unaofanywa na serikali dhidi ya wapigaji baada ya Moscow kupeleka majeshi huko Ukraine mwezi Februari 2022.

Shirika la habari la serikali ya Russia Tass lilisema kuwa iwapo mtu atakutikana na hatia chini ya sheria hiyo mpya, ni fedha, mali na rasilimali “zilizopatikana kupitia njia za uhalifu” au kutumika katika harakati didi ya usalama wa taifa wa Russia vingeweza kutaifishwa.

Bunge kandamizi katika enzi ya Soviet liliidhinisha utaifishaji wa nyumba kutokana na makosa mbali mbali ya jinai.

Forum

XS
SM
MD
LG