Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 04:16

Ukraine imesema vikosi vyake vilitungua drone 11


Russia Ukraine Map
Russia Ukraine Map

Kampuni ya nishati ya Ukraine, Ukrenergo imesema uharibifu ulitokea  katika vituo vyake na kupelekea umeme kukatika

Maafisa wa kijeshi nchini Ukraine wanasema Russia ilirusha darzeni mbili ya ndege zisizo na rubani usiku kucha ambazo zililenga miundombinu muhimu ya nchi hiyo na kukata umeme katika maeneo ya katikati mwa Ukraine, na kaskazini mashariki.

Kampuni ya nishati ya Ukraine, Ukrenergo imesema Ijumaa kwamba baadhi ya uharibifu ulitokea katika vituo vyake na kusababisha kukatika kwa umeme katika mji wa Kryvyi Rih katika mkoa wa Dnipropetrovsk. Shirika la habari la AFP liliwanukuu maafisa kaskazini mashariki mwa Kharkiv wakisema kuwa miji na makazi 64 pia yameachwa bila umeme kutokana na mashambulizi ya Russia.

Ukraine imesema vikosi vyake vilitungua drone 11. Wakati huo huo, Ufaransa imethibitisha Ijumaa kwamba wafanyakazi wawili wa kujitolea wa Ufaransa waliuawa Alhamisi katika shambulio la ndege isiyo na rubani la Russia karibu na mji wa Kherson kusini mwa Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG