Watu wengi wakiwa wamevalia rangi za kijani na dhahabu, ambazo ni rangi za timu ya taifa, walijaza kila nafasi iliyopatikana kwenye uwanja wa ndege wa OR Tambo kuwasalimia mabingwa waliovunja rekodi ya dunia kwa mara nne.
Afrika Kusini iliwashinda wapinzani wake wakuu New Zealand kwa 12-11 katika fainali kali iliyofanyika mjini Paris, Jumamosi iliyopita na kutwaa mataji mfululizo, walishinda mwaka 1995 na mwaka 2007 kutwaa taji la dunia.
Wafuasi walishangilia kwa pamoja wakati nahodha Siya Kolisi alipojitokeza hadharani, na kuwapungia mkono umati wa watu akiwa ameshikilia Kombe la Webb Ellis Cup, na kupiga picha za selfie na wafuasi waliokuwa wakishangilia.
Wengi walirusha vipeperushi vilivyoandikwa "Bokke [Springboks], kundi la washindi", huku sauti kubwa ya muziki ukipigwa pembeni na kuweka mandhari ya sherehe. Bendi ilipiga wimbo wa taifa.
Mafanikio haya ya karibuni, yameleta furaha kwa nchi hiyo inayopambana na ukosefu wa ajira, umeme, maji na migogoro ya uhalifu.
Rugby ni mojawapo ya michezo mitatu maarufu nchini Afrika Kusini, lakini ndiyo mchezo pekee unaoleta vikombe mara kwa mara.
Timu ya kandanda haijashinda tangu, iliposhinda Kombe la Mataifa la Afrika mwaka 1996 wakati upande wa kriketi bado haujashinda taji lolote la dunia.