UN yaanza uchunguzi baada ya Monusco kushutumiwa kwa mauaji DRC

Muathiriwa wa mapigano nchini DRC.

Umoja wa Mataifa umeanzisha uchunguzi kubaini kile kilichosabisha mauaji ya raia wanne wa DRC, huku ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo, Monusco, ukinyooshewa kidole.

Kasereka Kathavira, katibu mtendaji wa muungano wa mashirika ya kiraia katika eneo la Basongora akiwa katika Mji wa Kasindi Beni Kivu mpakani mwa Uganda na DRC chini ya Mlima wa Rwenzori, ni miongoni mwa watu ambao wamekutana na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, ambao wameanzisha rasmi uchunguzi kuhusu shutuma za mauji ya raia wakati wa maandamano ya kupimga uwepo wa MONUSCO.

Nate Giresse Kambale amekatwa mguu wake baada ya kupigwa risasi, na anashutumu kikosi cha Umoja wa Mataifa kilicho kasindi.

Your browser doesn’t support HTML5

voa oct 20 2022 uchunguzi wa UN waanza Beni (2).mp3

Mmoja wa waathiriwa wa DRC

Giresse amesema kwamba emewasamehe watu wa UN walio sababisha mguu wake kukatwa na kumuacha akiwa mlemavu anayetumia mguu mmoja.

Wengi wa wakazi wa eneo hilo wanasema hakukupata nafasi ya kukutana na wachunguzi wa UN ili kuwaeleza yaliowapata wakati wa maandamano yaliyopelekea watu wanne kupoteza maisha na zaidi ya nane kujeruhiwa kwa risasi

MONUSCO inatarajia kutoa ripoti yake baada ya uchunguzi huo ambao unandelea baada ya watu kaadhaa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa wakati wa maandamano ya kupinga uwepo wa MONUSCO nchini humo.

-Imetayarishwa na Austere Malivika, VOA, Goma, DRC