Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 05:27

UN yasema kundi la wakimbizi wa DRC waliokuwa Zambia wamerejea makwao


Shirika la kuhudumia wakimbizi katika Umoja wa Mataifa (UNHCR )
Shirika la kuhudumia wakimbizi katika Umoja wa Mataifa (UNHCR )

Umoja wa Mataifa ulisema Jumanne kwamba karibu wakimbizi 6,000 wa Congo waliokimbilia Zambia mwaka 2017 wamerejea nyumbani tangu kuzinduliwa kwa mpango wa kuwarejesha makwao kwa hiari hapo mwaka 2021.

Maelfu ya watu walivuka na kuingia Zambia kutoka jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo miaka mitano iliyopita, wakikimbia mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na makundi ya wanamgambo pamoja na mapigano ya kikabila.

Wakati baadhi ya maeneo ya Congo ikiwa bado sio salama, lakini hali katika baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na jimbo la kusini la Haut-Katanga, imetulia na kuruhusu kurejeshwa kwa wakaazi, shirika la kuhudumia wakimbizi katika Umoja wa Mataifa (UNHCR) lilisema.

Taarifa hiyo imesema kwamba Waliorejea ambao wengi wao walikuwa watoto, walisafirishwa kutoka makazi ya wakimbizi ya Mantapala kaskazini mwa Zambia hadi DRC kwa basi.

Wameelezea kufurahishwa na furaha ya kuweza kurudi nyumbani na wanatarajia kuungana tena na familia zao pamoja na marafiki na kuanza maisha yao upya, shirika hilo liliongeza.

Zaidi ya wakimbizi 11,000 waliandikishwa kurejea mwishoni mwa mwaka, shirika la Umoja wa Mataifa lilisema.

Takribani wakongo milioni moja wamepata makazi katika nchi jirani, huku Zambia ikihifadhi Zaidi ya wakimbizi 60,000 nanaotafuta hifadhi na wakimbizi wa zamani kutoka nchi jirani ya kaskazini.

XS
SM
MD
LG