Uganda ilipeleka wanajeshi wake nchini DRC mwezi Disemba mwaka jana kuisaidia nchi hiyo kupambana na waasi wa kundi la Alliance Democratic Forces (ADF).
Msemaji huyo wa jeshi la DRC ameiambia Reuters kwamba “ jeshi la Uganda halijatueleza mazingira ya ajali hiyo,” akiongeza kuwa imehusisha helikopta mbili.
Amesema ni watu 22 walifariki bila pia kupata maelezo zaidi.
Msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulayigye amethibitisha kwamba helikopta ya kwanza ilifanya ajali Jumatatu katika kijiji cha Boga jimbo la Ituri, huku helikopta ya pili ikianguka katika eneo la mpaka la Kabarole kati ya nchi hizo mbili.
Afisa mwengine amesema wanajeshi watatu wa Congo walifariki katika ajali ya kwanza, lakini hakikufafanua ikiwa walikuwa ndani ya helikopta au aridhini.
ADF ilianza kama kundi la uasi nchini Uganda lakini imekuwa na ngome zake nchini Congo tangu mwishoni mwa mwaka wa 1990.
Uganda ililishtumu kundi hilo kwa kuhusika katika mashambulizi matatu ya bomu mjini Kampala tarehe 16 Novemba mwaka jana, ambayo yaliua watu 7 wakiwemo washambuliaji wa kujitoa muhanga.