Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 19:33

Zelenskyy apeleka maombi mapya kuhutubia wakuu wa nchi wa AU


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki amesema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ametoa maombi mapya ya kuhutubia wakuu wa nchi katika Umoja wa Afrika.

Katika mtandao wa Twitter Faki alisema alipokea ombi wakati wa mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine.

Wawili hao pia walizungumzia kuhusu nia ya Rais Zelenskyy kutaka kuwa na ushirikiano wa karibu na Umoja wa Afrika.

Hata hivyo Faki hakutoa maelezo ya wazi kama ombi hilo litakubaliwa lakini alisisitiza katika mtandao wa Twitter kwamba kuna haja ya kupata suluhu ya amani kwa mzozo wa Russia.

Mapema mwezi huu Rais Zelensky alikuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Senegal Mack Sally mwenyekiti wa sasa wa AU na kuomba kuhutubia viongozi wa sasa.

Nchi za Afrika zilitawala katika orodha ya mataifa ambayo yalisusa kulipigia kura azimio la Umoja wa Mataifa la kuisimamisha Russia katika baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.

Azimio hilo lilipitishwa kwa kura 93 za ndio, 24 za kupinga na 58 hazikuunga mkono.

XS
SM
MD
LG