Hali ya mivutano imeongezeka wiki hii baada ya Moscow kuishutumu Uingereza kwa kile imekitaja kama kuichochea Ukraine kushambulia sehemu muhimu ndani ya Russia.
Russia imesema kwamba hatua hiyo itajibiwa kwa haraka sana na kwa uzito unaostahili.
Wallace amesema kwamba kulingana na sheria ya kimataifa, Ukraine ina haki ya kujilinda kwa kila namna.
Alisema kwamba kama sehemu ya kujilinda, Ukraine inaweza kushambulia sehemu ambazo Russia inaweka chakula, mafuta na risasi ili kumaliza uvamizi wa Russia.
Uingereza imekuwa ikiiunga mkono Ukraine tangu uvamizi wa Russia ulipoanza mwezi Februari, na imekuwa ikutuma misaada ya silaha kwa Ukraine kuisaidia kupambana na Russia, japo imesema kwamba haitatuma makombora ya masada marefu kwa Ukraine.