Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 11:37

Kombora lililorushwa na majeshi ya Russia laua mwandishi wa habari mjini Kyiv

Mwandishi wa habari wa Radio RFE/RL Vira Hyrych kutoka ukurasa wake wa Facebook.
Mwandishi wa habari wa Radio RFE/RL Vira Hyrych kutoka ukurasa wake wa Facebook.

Russia imemuuwa mwandishi wa habari kutoka kituo cha utangazaji kinachoungwa mkono na Marekani cha Radio Liberty katika shambulio la Kombora dhidi ya Kyiv.

Shambulio hilo limefanyika wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa Ukraine shirika hilo la utangazaji limesema Ijumaa.

Radio Free Europe / Radio Liberty yenye makao yake mjini PRAG ilisema mwili wa mtayarishaji wa vipindi Vira Hyrych ulipatikana Ijumaa asubuhi katika kifusi baada ya shambulizi la Alhamisi lililoharibu ghorofa mbili za chini katika jengo la makazi ya watu.

Imesema Hyrych amefanyakazi katika Radio Liberty tangu mwaka 2018.

Waokoaji wakiwa wamebeba mwili wa mwandishi wa habari wa kituo cha Radio Liberty Vira Hyrych, aliyeuawa na shambulizi la angani lililoharibu jengo la makazi, wakati Russia ikiendelea na uvamizi wa Ukraine, mjini Kyiv, Ukraine Aprili 29, 2022.REUTERS/Gleb Garanich.

Radio hiyo inayofadhiliwa na Marekani, ambayo iliandika habari za umoja wa Soviet ya zamani tangu vita baridi , ni moja ya vyanzo vya habari vya Russia vilivyosalia vya lugha ya Russia nje ya udhibiti wa Kremlin, tangu Moscow ilipofunga vyombo vya habari binafsi ndani ya Russia kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine February 24.

Makombora yalipiga mji mkuu wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres .

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksiy Reznikov ameliita shambulizi dhidi ya usalama wa katibu mkuu na usalama wa dunia.

XS
SM
MD
LG