Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 01:55

Wizara ya Ulinzi : George H.W. Bush kuagwa kwa heshima zote za kitaifa


 Rais George H. Bush akijipiga picha ya selfie akiwa na wanajeshi wa majini uwanja wa ndege wa Baidoa, Januari 1, 1993, Baidoa.
Rais George H. Bush akijipiga picha ya selfie akiwa na wanajeshi wa majini uwanja wa ndege wa Baidoa, Januari 1, 1993, Baidoa.

Maelezo zaidi juu ya mipango ya maziko ya Rais mstaafu George H. W. Bush, ambaye aliaga dunia Ijumaa akiwa na miaka 94, yanaandaliwa na familia ya Bush, Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza Jumamosi.

Bush ambaye alitumikia nafasi ya urais tangu mwaka 1989-1993, ataagwa kwa heshima zote za kitaifa Jumatano katika Kanisa la Cathedral, Washington na kuzikwa Alhamisi katika maktaba yake ya urais huko Texas.

Baada ya maandalizi hayo kuwa tayari katika makao makuu ya taifa Jumatatu, mwili wake utawekwa katika ukumbi wa Rotunda ndani ya Bunge la Marekani kwa ajili ya wananchi kuja kuuaga mpaka Jumatano asubuhi, wakati utaratibu kupewa heshima zote za kitaifa uliondaliwa saa kumi na moja jioni (majira ya Marekani) Jumatatu.

Umma wa Wamarekani utaweza kuendelea kutoa heshima zao za mwisho wakati mwili wa Bush ukiwa katika jeneza kuanzia Jumatatu kuanzia saa moja na nusu asubuhi (majira ya Marekani) hadi Jumatano saa moja asubuhi.

White House imetangaza Jumamosi kuwa Rais Donald Trump wa Marekani atahudhuria shughuli za kuuwaga mwili wa Bush kitaifa.

Msemaji wa White House Sarah Sanders amesema katika tamko lilitolewa kwamba Jumatano imepangwa kuwa siku ya kitaifa ya maombolezi, na bendera ndani ya White House tayari zimeshushwa nusu mlingoti kumuenzi Bush.

XS
SM
MD
LG