Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 12:57

Tanzia: Historia itakavyo mkumbuka Rais George Herbert Walker Bush


Rais George Herbert Walker Bush
Rais George Herbert Walker Bush

Rais wa zamani wa Marekani, George Herbert Walker Bush amefariki nyumbani kwake huko Houston, katika jimbo la Texas. Alikuwa na umri wa miaka 94.

Alikuwa rais wa 41 wa Marekani, Mrepublican ambaye alihudumu kwa kipindi kimoja kuanzia mwaka 1989 mpaka 1993. Anakumbukwa kwa kuwavamia wanajeshi wa Iraq waliokuwa nchini Kuwait na kwa juhudi zake katika mkatabab wa amani wa Mashariki ya Kati.

Wakati jeshi la Iraq lilipojiingia nchini Kuwait Agosti ya 1990, Bush aliunda ushirika wa kimataifa wa majeshi ya anga na ardhini ili kuikomboa nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta na kutoa uhakikisho wa Salama kwa washirika wake katika eneo la ghuba. Operesheni ya kuikomboa Kuwait ilianzishwa Januari yam waka uliofuata.

“Miezi mitano iliyopita, rais wa Iraq, Saddam Hussein alianza vita vya kikatili dhidi ya Kuwait. Hivi leo, tumejiunga katika mapambano,” alisema rais wa 41 George H.W. Bush.

Operesheni Desert

Iliyoongozwa na Marekani iliyasukuma majeshi ya Iraw nje ya taifa hilo katika muda wa wiki sita na Bush alifanya maamuzi ya kuacha vita. Wengi walikosoa maamuzi hayo wakisema yalikuwa ni Mapema mno, lakini heshima ya Bush nyumbani na kwingine iliongezeka. Alitumia fursa hiyo kuimarisha tena utaratibu wa amani kati ya waarabu na waisraeli, na juhudi hii ilisababisha kuwepo kwa Madrid Conference baadaye mwaka huo huo.

Jaribio lake la kurejesha utaratibu katika nchi iliyokumbwa na vita vyaSomalia. Mwezi Desemba 1992, katika wiki za mwisho za urais wake, halikuwa na mafanikio na mapigano yaliendelea mpaka wakati wa urais wa Clinton.

Bush alimrithi Rais Ronald Reagan mwaka 1989, baada ya kuhudumu kwa vipindi viwili kama makamu wa rais. Urais wake uliona mabadiliko makubwa yakitokea duniani, kuanzia kuanguka kwa ukuta wa Berlin katika mwaka wake wa kwanza ofisi. Halafu kuvunjika kwa Umoja wa Sovieti mwaka 1991 na Bush na rais wa mwisho wa Soviet, Mikhail Gorbachev walitangaza ushirika wa kimkakati kati ya Marekani na Russia na kuashiria kumalizika kwa vita baridi.

Lakini nyumbani,Bush aliwasikitisha wapiga kura pale aliposhindwa kutekeleza ahadi yake ya kampeni ya kupunguza kodi.

Rais mrepublican alilazimishwa na wademocrat walio wengi katika Bunge kupandisha kodi ya mapato ili kuzuia kuongezeka kwa nakisi Katika bajeti. Kudorora kwa uchumi na maswali mengi kuhusu vita vya ghuba kulichangia kuanguka kwa viwango vyake vya utendaji na hivyo kushindwa kuchaguliwa tena mwaka 1992.

Baada ya kushindwa Bush alistaafu katika siasa na kwenda kuishi Texas, ambako alijipatia utajiri kutoka na biashara ya mafuta. Lakini hakupotea katika jicho la umma. Aliingia tena katika harakati za kisiasa wakati wa kampeni ya mtoto wake miaka minane baadaye.

Katika moja ya mikutano ya kampeni, rais wa 41 alisema huvu mwanamme, ni mtoto wetu na hatawaangusha. Atakuwa na nyinyi wakati wote na atawahudumia kwa heshima kubwa.

Mwaka 2005, kwa ombi la mtoto wake George, ambaye alikuwa rais wa 44 wa Marekani, Bush mkubwa aliuangana na hasimu wake wa zamani Bill Clinton katika juhudi za kuwasaidia waathirika wa kimbunga Katrina.

Miongoni mwa heshima mbali mbali, alizopokea tangu wakati huo ni medali kutoka kwa malkia wa Uingereza Elizabeth na medali ya uhuru kutoka kwa Rais Barack Obama.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Khadija Riyami, Washington, DC

XS
SM
MD
LG