Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:28

Seneta McCain kuzikwa katika chuo cha jeshi la majini


Kitabu cha Senata John McCain, kimewekwa juu ya bendera ya Marekani katika viwanja vya mashujaa wa Vietnam vya taifa, Septemba 1, 2018.
Kitabu cha Senata John McCain, kimewekwa juu ya bendera ya Marekani katika viwanja vya mashujaa wa Vietnam vya taifa, Septemba 1, 2018.

Siku tano za maombolezo ya Seneta aliyeaga dunia John McCain zina malizika Jumapili wakati atakapo zikwa katika eneo la makaburi ya mashujaa wenzie, huko katika Chuo cha Mafunzo ya askari wa majini cha Marekani, Naval Academy, mji mkuu wa Maryland, Annapolis, jirani na mji wa Washington.

Sehemu atakapo zikwa Mrepublikan huyu wa Arizona, ambaye alifariki Jumamosi akiwa na umri wa miaka 81, itakuwa pembeni ya kaburi la rafiki yake wa muda mrefu na mwanafunzi mwenzie akiwa jeshini, Admirali Chuck Larson, aliyekufa mwaka 2014.

McCain, ambaye ni rubani mstaafu aliwahi kuwa mfungwa wa kivita baada ya kutekwa Vietnam na kushikiliwa kwa zaidi ya miaka mitano.

McCain alifanya ziara yake ya mwisho katika chuo hicho mwezi Octoba, na kuwaambia wanafunzi kwamba chuo hicho kilikuwa kimemtayarisha hata kupambana na changamoto ambazo bado hajawahi kukutana nazo.

Katika ibada iliyo andaliwa na familia ya kumuaga McCain Jumamosi huko katika kanisa la kitaifa la Cathedral, Washington, Rais mstaafu Barack Obama alimpongeza McCain, rafiki yake na wakati fulani akiwa mpinzani wake wa kisiasa, kwa kusema McCain aliwapa moyo Wamarekani wote “kufikia ubora zaidi, kutenda mambo bora zaidi, kujenga sifa zile walizoturithisha waasisi wa taifa letu.”

“Sehemu kubwa ya siasa zetu, maisha yetu ya umma, na hotuba zetu kwa umma zinaweza kuonekana kama ni jambo dogo, likisambaza malumbano ya majivuno, matusi na ulaghai na kusababisha uhalifu,” amesema Obama.

Bila ya kumtaja Rais Donald Trump kwa jina, Obama ameongeza, “ ni siasa zinazo fungamana na ulaghai wa ujasiri na misimamo, lakini ukweli ni kuwa zinatokana na uwoga. John alituhimiza kuwa zaidi ya hapo, alitoa wito kwetu tuwe bora zaidi kuliko hayo.

Katika ujumbe wake wa tanzia Mrepulikan mwenzie McCain, Rais mstaafu George W. Bush amesema McCain “alikuwa muungwana, siku zote akitambua kuwa wapinzani wake walikuwa bado ni wazalendo na binadamu wenzie.”

Bush amesema hakubaliani na hali ya siasa za Washington, jambo ambalo amesema siasa hizo ni kinyume kabisa na imani binafsi ya McCain.

“Amesema McCain aliheshimu utu wa kila binadamu, utu ambao hauishii katika mipaka na ambao madikteta hawawezi kuutokomeza,” Bush amesema. Pengine juu ya yote hayo, John alikerwa na utumiaji mbaya wa madaraka.”

Bush na Obama walikuwa wamekaribishwa kuja kutoa tanzia ya rafiki yao katika ibada hiyo, ambayo ilikuwa imeandaliwa na McCain mwenyewe wakati akipambana na maradhi ya saratani ya ubongo. McCain alishindwa katika chaguzi mbili, kwanza katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa urais ndani ya chama chake aliposhindana na Bush mwaka 2000, na pili katika uchaguzi mkuu wa urais alipogombea na Obama mwaka 2008.

XS
SM
MD
LG