Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:00

WHO yaomba msaada kuziokoa nchi 54 zinazo kabiliwa na dharura ya janga la afya


Tedros Adhanom Ghebreyesus
Tedros Adhanom Ghebreyesus

Shirika la Afya Duniani linaomba msaada wa dola billioni 2.54 ili kuwasaidia  mamilioni ya watu katika nchi 54 zinazokabiliwa  na dharura ya janga la afya  lililosababishwa  na maafa mengine ya kiasili na yanayotokana na binadamu.

Katika uzinduzi wa ombi hilo, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema ulimwengu unashuhudia mkusanyiko wa migogoro isiyotarajiwa ambayo yanahitaji hatua ambazo hazijawahi kuchukuliwa.

Amesema WHO inashughulikia idadi kubwa sana ya matukio ya dharura ya kiafya yanayoingiliana. Haya ni pamoja na mafuriko yanayohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa nchini Pakistani , ukame na njaa kali kote katika eneo la Sahel na eneo kubwa la Pembe ya Afrika, changamoto za kiafya zilizo sababishwa na vita nchini Ukraine , na milipuko ya surua, kipindupindu na magonjwa mengine yenye kuua katika darzeni za nchi.

“ Dunia haiwezi kupuuzia ikitumaini matatizo haya yatajitatua yenyewe” Tedros alisisitiza “kwa ufadhili na hatua za haraka , tunaweza kuokoa maisha, kuunga mkono juhudi za uponyaji na kuepusha kusambaa kwa magonjwa ndani na nje ya mipaka , na kuzisaidia jamii na kujenga upya fursa kwa mustakbali wao.

WHO inaripoti asilimia 80 ya mahitaji ya kibinadamu duniani yanachochewa na migogoro, na karibu nusu ya vifo vya uzazi na watoto vinavyoweza kuzuulika vinatokea katika hali tete, kwenye mazingira yaliyoathirika na migogoro na hatarishi.

Kanda ya Afrika inakabiliwa na mzigo mkubwa wa dharura za afya ya umma ulimwenguni. Mwaka 2022, bara hilo lilihusika na asilimia 64 ya huduma zote za dharura za daraja la 3, au hali mbaya kabisa, dharura mbalimbali za kimataifa.

Kwa sasa WHO inasaidia migogoro 54 ya kiafya ikiwemo 11 iliyoorodheshwa kuwa ya daraja la 3. Inajumuisha nchi saba za Afrika ikiwemo Afghanistan, Syria, Ukraine, and Yemen.

XS
SM
MD
LG