Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:21

WHO: watu wengi wanafariki China kutokana na Corona


Waafiri wakipita karibu na kituo cha kupimba virusi vya Corona katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Incheon, Korea kusini. Jan 10, 2023 China imepiga marufuku wasafiri kutoka Korea kusini
Waafiri wakipita karibu na kituo cha kupimba virusi vya Corona katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Incheon, Korea kusini. Jan 10, 2023 China imepiga marufuku wasafiri kutoka Korea kusini

Shirika la Afya duniani limesema Jumatano, limeitaka China kutoa taarifa kuhusu ongezeko la maambukizi ya Covid 19 .

“WHO bado inaamini kuwa kuna vifo vingi vinavyotokea China lakini haviripotiwi, hii pia inahusiana na ufafanuzi unaotumika, lakini pia kwa mahitaji ya madaktari na wale wanaotoa taarifa kwenye mfumo wa afya ya jamii watiwe moyo kuripoti visa hivi na siyo kukatishwa tamaa” Mkurugenzi WHO Michael Ryan, aliwaambia waandishi wa habari.

Ryan ameipongeza China kwa juhudi za kuongeza idadi ya vitanda katika vyumba vya wagonjwa mahututi na utumiaji wa madawa ya kuzuia virusi katika hatua za mwanzo za matibabu.

Ukosefu wa takwimu sahihi kutoka China, umepelekea nchi nyingi kuweka masharti ya upimaji wa wasafiri kutoka China.

“Ukofefu wa takwimu, baadhi ya nchi zimefanya uamuzi wa kuchukua tahadhari na WHO imesema kuwa hayo ni mazingira yanayoeleweka” Ryan amesema .

XS
SM
MD
LG